Nimegundua kitu kuhusu hizi placements.
Yaani zinapitia hatua ndefu hadi zije zitoke ndio maana tunaona zinachelewa sana.
Barua zetu zimeandikwa tarehe 8/12/2022(mwezi mmoja baada ya Oral) halafu placement imetoka tarehe 9/1/2023(mwezi mmoja baada ya barua kauandaliwa).
Je hiyo interval ya mwezi mmoja mmoja, nini huwa kinafanyika?
Turejee kanuni zao.
Baada ya Oral matokeo hukusanywa/alama zinakusanywa zinakuwa compile sehemu moja kama oral ilifanyika sehemu tofauti tofauti(yaani PSRS na Zenji). Then Mwenyekiti wa jopo la Panelist atakabidhiwa hayo matokeo na yeye atayawasilisha kwenye Board ili placement zikapangwe kulingana na ufaulu wa oral.(hapo mwezi ushakatika).
Mwezi mwingine inakuja suala la kusainiwa, Hapa mzee Kitenge atatenga muda wa kuzisaini barua zote zilizoandaliwa, hadi kumaliza mwezi ushakatika.
Baada ya hapo ndio zamu ya placements inafika, ikitoka tu barua ziko tayari ndio maana kuchukua barua haichukui muda ni dk chache tu.
Kwa hiyo mnaosubiri placement inabidi mtambue hilo na subira ndio silaha ya kuishi nayo katika hicho chote