Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ni kweli mkuu ila utumishi bhana sidhani kama kwenye mavazi wanazingatia...

Aaah hilo ndo la kwanza ukiingia tu pale kwenye room ya interview supervisor wa utumishi ndo kazi yake hiyoo ya kwanza then anandika marks zake na report ya muonekano wako.

Wanazingatiaa vibaya mno, last interview nlienda kuna mwana alivaa sandals kuna msimamizi anaeita majina anakupeleka machinjioni akamuona kumuuliza vipi jamaa akadai anaumwa miguu akamwambia kule ndani hutumii zaidi ya dakika 15 tafuta viatu uvae ukitoka we endelea na sandals.

Na yeye ndo akatwambia mchanganuo wa marks sio maswali pekee kuna vitu vingine wanaangalia na kukupa marks, sometimes mtu anayumba kwenye maswali ila huku kwingine kunambeba ndo anaanza kushangaa nimepataje na skujibu vizuri maswali.
 
Huu ufafanuzi umemaliza kabisa.Somo limeeleweka.
 
Vingine tunaviomba hapa please, please
 
Sawa, na wewe unajua nini kuhusiana na hilo bila ubishani ili usaidie tusiojua?
Nilichobishia mimi ni hilo la kusema eti tai nyekundu inapunguza marks ndio nikatolea mfano huyo mdau niliyemuazima tai nyekundu na akafanikiwa kupata nafasi..hilo la kwenda ukiwa smart sijalibishia..
 
Hellow wasaka mirija ya asali wenzangu, nimeitwa MUST IT technician, nikiwaza gharama ya dar to mbeya kwa one POSt nachoka, heri ingekuwa DOM, waja Leo waondoka Leo. Huku Si nikukomoana na wanajua hatuna mitaji.
 
Nafasi katika hiyo post zilipunguzwa mpaka kubaki moja baada ya kufunga maombi ya usaili au wakati majina ya "shortlist" ya usahili yanatolewa?

Na je, wakati wa kutuma maombi zilikua nafasi ngapi katika hiyo post mpaka ukashawishika kuomba mkuu?
 
Nilichobishia mimi ni hilo la kusema eti tai nyekundu inapunguza marks ndio nikatolea mfano huyo mdau niliyemuazima tai nyekundu na akafanikiwa kupata nafasi..hilo la kwenda ukiwa smart sijalibishia..
Ulimuazima sawa ila hujui kama alivaa akaingia nayo au hakuvaa maana haukuwa nae kwenye saili. Ila jua tu Tie ya rangi nyekundu ni ya mamlaka haishauriwi kuvaa kwenye occasions kama hizo. Umeshauriwa ila ukiona sio kweli we vaa kwenye usaili wako ukifanikiwa kufika oral
 
Me nadhani wewe umesimuliwa tu basi ukalichukua kama lilivyo.anyway kila mtu aamimi anavyoamini hakuna haja ya kubishana kwenye hilo.
 
Nafasi katika hiyo post zilipunguzwa mpaka kubaki moja baada ya kufunga maombi ya usaili au wakati majina ya "shortlist" ya usahili yanatolewa?

Na je, wakati wa kutuma maombi zilikua nafasi ngapi katika hiyo post mpaka ukashawishika kuomba mkuu?
Ha ha ha,maswali yana akili haya.huenda jamaa alitegemea ataitwa mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…