smurof
Senior Member
- Feb 25, 2022
- 103
- 293
Ni kweli mkuu ila utumishi bhana sidhani kama kwenye mavazi wanazingatia...
Aaah hilo ndo la kwanza ukiingia tu pale kwenye room ya interview supervisor wa utumishi ndo kazi yake hiyoo ya kwanza then anandika marks zake na report ya muonekano wako.
Wanazingatiaa vibaya mno, last interview nlienda kuna mwana alivaa sandals kuna msimamizi anaeita majina anakupeleka machinjioni akamuona kumuuliza vipi jamaa akadai anaumwa miguu akamwambia kule ndani hutumii zaidi ya dakika 15 tafuta viatu uvae ukitoka we endelea na sandals.
Na yeye ndo akatwambia mchanganuo wa marks sio maswali pekee kuna vitu vingine wanaangalia na kukupa marks, sometimes mtu anayumba kwenye maswali ila huku kwingine kunambeba ndo anaanza kushangaa nimepataje na skujibu vizuri maswali.