Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hv jamani mbona PSRS hawatoi tena MIKEKA ya Usaili.. naona kimya Toka ilivyopita Ile ya Bunge na huu mwaka unaisha.. Sa inafikia kipindi inakubid Kila siku uwe na bando ili uweze kuona kama call for interview imetoka..

Aisee Mkuu, leo nilikuwa eneo fulani akawepo mkuu wa chuo fulani hapa Dar, yule Proff alikuwa analalamika namna Utumishi wanachelewesha sana kuwatimizia hitaji lao.

Anadai walipeleka madai ya watumishi 50 tangu mwezi February, na walipanga kwamba mpaka sasa wangekuwa wameshawapata hao walimu ili wawe na uhakika wa kuanza nao mwaka mpya wa masomo 2022/2023, ila cha ajabu ndio kwanza wanahangaika na written.

Mpaka akafikia kusema, aliwashawishi sana, waache chuo chenyewe kisimamie ila Utumishi wakagoma.


Hapa ndipo nikaamini tatizo haliko kabisa kwenye taasisi zenye mahitaji, liko Utumishi.
 
Back
Top Bottom