Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Nasikia uchungu Sana wapambanaji wenzangu ambao Bado hamjapata nafasi...ila ukweli NI kwamba Huku makazini wazee wengi wanastaafu so Ajira Lazima TU wawepo wa kureplace.komaeni Sana na data na vifaa kutegemea na fani yako...of course me nimeingia kwa Utechnian sijui mwenzang kada yako nini
Mungu akubariki zaidi kiongozi
 
Nimepitia kwenda oral dah kwenye account tayari ngoja nisubr mkeke sijui nimepata hamsin na ngapi duh utumishi wamedandia mtumbi wa vibengo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hongera sana, hukuamini ila maajabu yakawa upande mzuri.

Oral ni hatua muhimu sana, kapambane
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ni noma kumbe now ni mwendo wa kujitungia tu majibu unaweza ukafaulu tu aisee usiache swali kwa kweli
Kada zingine kama Afya kutunga majibu ni kazi. Jibu kama ni mdudu fulani, ukijitungia mdudu mwingine unakandwa bila huruma[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aisee Mkuu, leo nilikuwa eneo fulani akawepo mkuu wa chuo fulani hapa Dar, yule Proff alikuwa analalamika namna Utumishi wanachelewesha sana kuwatimizia hitaji lao.

Anadai walipeleka madai ya watumishi 50 tangu mwezi February, na walipanga kwamba mpaka sasa wangekuwa wameshawapata hao walimu ili wawe na uhakika wa kuanza nao mwaka mpya wa masomo 2022/2023, ila cha ajabu ndio kwanza wanahangaika na written.

Mpaka akafikia kusema, aliwashawishi sana, waache chuo chenyewe kisimamie ila Utumishi wakagoma.


Hapa ndipo nikaamini tatizo haliko kabisa kwenye taasisi zenye mahitaji, liko Utumishi.
Hilo kweli maana tumeona Vyuo wanaendesha michakato ndani ya mwezi mmoja then watu wanakabidhiwa Cheque number
 
Ratiba ya sahili inaisha mwezi huu mwishoni. Mikeka ya sahili ilipotoka kuanzia tarehe 30, August tarehe zilipangwa hadi mwezi huu uishe.

Kwa sasa mikeka maarufu iliyobaki ni MGA & LGA, NAOT, Legal(kama sikosei), TRA, MUHAS n.k, hii ni mikeka mikubwa naitabiria kupangiwa ratiba kuanzia mwezi ujao.

Hahaha, Mkuu umechambua Kitaalamu sana.
 
Back
Top Bottom