Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hili ni sahihi sana, ni wazi wameshindwa kutekeleza ahadi walizoahidi wateja wao.
Wana uhaba wa watendaji, hizi nyomi zinahitaji wachakataji wa kutosha.

Ebu fikiria zile nafasi za Legal zilikuwa zaidi ya 100, na hapo zikiwa nyingi waombaji wanakuwa wengi zaidi kwa sababu kila mtu anakuwa na matumaini ya kupata nafasi kwa kuwa zipo nyingi, mwisho wa siku unakuta maombi mengi sana.
 
Noma mkuu mwezi huu na miwili inayokuja inaweza kuisha kabisa bila shida na Bado tukawa mtaani tu duh process kubwa sana Yan ndo kwanza una lipoti makao makuu then wachakate ndo upangiwe kituo cha kazi dah[emoji23][emoji1787] mie interview ikijaa naenda kudadeki na placement nyingine ikitoka sijui itakuaje aiseee
Copy kibao za vyeti wanataka mia kasoro, mara hostiptal check up, nida copy,bank copy hahaahahahahhaa nimeenda kufanya check up Sina ugojwa namaliza process zote Nishapata ugojwa wa ulemavu wa miguu nimetembea mpka nimekoma
Hahahahaa, omba Mungu usipate kashkash itakayokukwamisha, upo hatua za mwisho za kufunga mrija wa Asali, ukimaliza kaa kwenye kiyoyozi uanze kuifyonza Asali taratibu.

Shortlist zinachukua muda mrefu

Placements zinachukua muda mrefu

Taratibu za kuungwa kwenye Mrija na Mwajiri zinachukua muda mrefu.

Ukishaungwa kwenye mrija, unaweza kukuta ukacheleweshewa kuanza kupata Salary(hii ishu ni common kwa beginner)

Tabu tupu!
 
Back
Top Bottom