Haya mambo haya, naomba nitoe ushuhuda, me kipindi nipo chuo nlikuwa na hela mno, ni hivi vibiashara vyangu na kidogo walezi wangu walikuwa vizuri na elimu wanaithamini sana. Nlikuwa na boy friend wangu akiniomba 5000, 10,000 sion shida kumpa. Kidogo kwao hawakuwa vizuri na yeye ndo first born, vitu vya ndani nanunua nampa, akija hostel namchambulia vitu nampa, hadi nlimpa jiko la umeme awe anapikia kwake maana chuo warden alikaza. Inshort nlimbeba sana. Nauli za chuo nampa hapo yeye ndo anasoma CPA. Aisee baadae akalamba asali bana TRA, kama custom officer, na mimi nkamaliza chuo maisha yakanipiga, akabadilika kabisa kabisa, nkawa nalia na mapenzi wee[emoji23][emoji1787], akahamishiwa Dar nkahisi labda shida ilikuwa long distance rship, Dar wakamuweka TPA, aisee na mapenzi yakaisha kabisa na mimi nkasema hamna changu hapa, kama ni pesa najua kuitafuta. From then aisee nkajisemea kumbe haya mambo sio ya wadada peke yao. Ata mdada unaweza mvumilia jobless mwenzio hapa akilamba asali tu ndo anakuonaje sijui [emoji1787]. Kikubwa upendo tu.