Sijui hili linatawaliwa na njia inayotumika sasa hivi???? sidhani hata kidogo, kuna mifano mingi watu walifanyiwa usahili wakachukuliwa wachache na kuwakuta wenzao wameanza kazi siku nyingi wala hawakufanya interview yenyewe. Hata hao waliopo huko wanaweza kupewa rushwa na upendeleo unaouzungumza ukafanyika. This is TZ bana!!!!!.
Tulitoka huko na kulikuwa na sababu lukuki kwa nini entities zinazotaka mfanyakazi kuhusika/ku-recriuit staff wao, miaka ile ya Structural adjustment haya yalipendekezwa na kutekelezwa kwa kipindi kirefu, kilichotakiwa sio kurudi kwenye cetralization rather tungeuboresha. Mwenye kujua staff anaemtaka ni employer/entity inayotaka kuajiri sio wale huko. Kingine nilichokiona ni sababu za kisiasa zaidi kuliko uhalisia na kuzungumzia upendeleo wa kindugu n.k. Siku hizi post zote zimekuwa za kisiasa wakurugenzi wa halmashauri/ majiji nk. wamekuwa makada wa chama pendwa kwa malengo ya kushinda uchaguzi na kutoka kwenye mfumo uliopendekezwa na UNDP miaka ile. Sababu nyingine ni siasa tu na sio nepotism. Hata makarani wa Sensa walitembea na vimemo vya chama pendwa ili waajiriwe acheni hii.