Sio rahisi kihivyo, ukiingia ndio utanielewa, kuhama sehemu moja kwenda nyingine hasa kwa watu walioko Dunia ya Giza kama hizo wilaya na kule Uvinza, Kibondo + Buhingwe ni ngumu kuhamishwa.
Hata kama una njaa, weka malengo yako ya kugombania kazi nzuri. Ukijipanga na ukisoma unaweza kufaulu mitihani ya utumishi.
Tangu kusoma kwangu, sijawahi kuomba kazi kwenye Halmashauri yoyote ile, sikutaka na nilipambana na mashirika ambayo mostly utakaa sehemu kidogo yenye unafuu wa mshahara na mazingira yako.
Mfano. MWALIMU WA BUHIGWE AU KONGWA anafanana na Mwalimu wa Dar au mikoa iliyoendelea kiasi? Kwann hawa wasipewe posho ya mazingira magumu? Vumbi, ukame, maji shida, umeme mtihani, usafiri mashaka nk, kwnn hawa wanaoishi zama za kale za mawe wasionwe na serikali kwa kuwapa posho ya mazingira magumu kutokana na utayari wao wa kulitumikia taifa wakiwa huko kusikonoga CHAI?