Hello jamani hivi ukiingia interview ya oral ukifik mle ndni unakaa kwenye kiti na unasalimia au untakiwa uambiwe kwnz then ndio ukae na waanze kukusalimia wao....na je swli la kwnza la explain about your self unaelezea mambo gani
Kikawaida unawasalimia kwanza, sa nyingine watanza kukusalimia wao ukiingia tu na kukuambia karibu ukae, wewe unaseama asante hivyo...hakuna formula cha muhimu ni kusoma mazingira chap chap na kufanya maamuzi sahihi
usiwaogope, ni binadamu, cha muhimu jiandae kwa kujua mambo muhimu ya hiyo taaisisi na vitu vya muhimu kwa kada yako
explain about yourself wanaeza kukuelekeza vya kusema kama wasipokuelekeza
1. jitambulishe majina yako
2. kada yako kama ni mchumi, ni mhandisi, nk
3. elimu yako kuanzia primary, secondary, chuo
4. uzoefu wako kama kuna kazi uliwahi fanya na linganisha uzoefu wako na zile job descrpition mfano kama job descrpition mojawapo ni kuandaa ripoti za matumizi bas utasema niliwahi fanya kazi ya field chuo nilikua nasaidia/nandaa ripoti, pia baada ya kumaliza chuo nilifanya internship nilifanya kazi ...unazitaja....zinazoendana na mahitaji ya kazi hii kwa hio naamini uzoefu wangu huu utanifanya kuwa chaguo bora kabisa la hii kazi
kisha unaeza kuongezea hobby zako ambazo zinakupa ubora zaid mfano hobby yako ni kusoma vitabu basi unaeza toa mfano kuwa ulisoma kitabu flani kuhusu kitu flani kikusaidia kuwa bora au unapenda kujiendeleza kwa kusoma majarida yanayohusu kada yako nk
5.
KUMBUKA YOTE HAYO NI KWA LUGHA YA KIINGEREZA. (unless otherwise) Kwa hio inabid ufanye mazoezi kama lugha hiyo sio lugh mama!
6. Omba sana, fanya yako mengine muachie Mungu.
kuwa na imani kama ipo ipo tu!