Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Yes ndio ilivyo sasa hivi unaona 1M kwa mwezi kubwa ila ukianza ipata ndio unajua hamna kitu.

By the way Lijendi uzi wako ule siku hizi kama umepoa hivi. Au ni sababu ya WC na mgao?
1M Ni ndogo Sana baada ya makato unajikuta 700k au Kama una mkopo unapata mpaka 600k na vipointi yaani unajikuta una hela za kuunga unga
 
Mwanangu Mwifwa nazan umetegesha sikio vzr la RECEIVED NA SHORTLISTED,na la KOMBE LA DUNIA [emoji23][emoji23]
Hahahaaa.

Received na Shortlist nishazimaliza.

Sasahivi ubao unasomeka Not Selected for Oral Interview.

Moja tu ambayo imenipa matumaini ilikuwa Selected for Oral Interview, ila tangu matokeo ya kuitwa Oral tarehe 4 Novemba, sijachungulia Status na nimeapa sitaiangali hadi pdf ya Asali itakapotoka
 
Ni mkubwa mwenzetu kiumri ila kiakili mtu wa miaka 25/26 wa miaka kadhaa iliyopita sio sawa na wa sasa katika hekima na busara
Nakubaliana na wewe, kipindi nipo mdogo, watu waliokuwa na umri huo walikuwa ni watu wazima kweli kibusara na kiakili
 
Voda Wana akili sana eti wamenipa mb 200 na nilikua Sina mb huwa natumia Airtel siku zote nashangaa napata sms una mb 200 na dakika 15
Basi Leo placement zinakuja
Mimi pia walinipa siku chache zilizopita, sikujua maana sikupokea sms ila nikaja kujua ambapo nilikuwa naangalia salio kwani nilitaka nitumie NMB mobile maana bila kuwa na salio la kawaida huwezi kuitumia.

Baada yakubonyeza menu nikalezewa sms ikisema sina salio la kawaida ila Mb, dk na sms zikawa zipo.

Nikajisemea kumbe mara nyingine huwa wanawajali Jobless, nikaanza kuzitumia, ziliiexpire baada ya siku kama 5 hivi
 
1M Ni ndogo Sana baada ya makato unajikuta 700k au Kama una mkopo unapata mpaka 600k na vipointi yaani unajikuta una hela za kuunga unga
Noma sana mkuu kutoboa hapo inahitaji heshima na nidhamu ya hali ya juu sana Kwa sie tusiokuwa na wakutugemea wengi unaweza pambana usave 400k kila mwezi ila utachakaa sana nakuambia
 
Hivi wakuu nikishapata Ajira baada ya muda gani naweza kuchukua mkopo, nivute ndinga.

Wanasema ukitaka jambo likutokee anza kabisa kulipangia mahesabu.
Mimi sijapata ajira ila nimeshaanza kuweka mipango.
 
Mimi pia walinipa siku chache zilizopita, sikujua maana sikupokea sms ila nikaja kujua ambapo nilikuwa naangalia salio kwani nilitaka nitumie NMB mobile maana bila kuwa na salio la kawaida huwezi kuitumia.

Baada yakubonyeza menu nikalezewa sms ikisema sina salio la kawaida ila Mb, dk na sms zikawa zipo.

Nikajisemea kumbe mara nyingine huwa wanawajali Jobless, nikaanza kuzitumia, ziliiexpire baada ya siku kama 5 hivi
Mie sms sikuisikia imeingia kimya kimya naenda kwenye sms ndo naiona nikasema Asante sana
 
Hivi wakuu nikishapata Ajira baada ya muda gani naweza kuchukua mkopo, nivute ndinga.

Wanasema ukitaka jambo likutokee anza kabisa kulipangia mahesabu.
Mimi sijapata ajira ila nimeshaanza kuweka mipango.
Sijajua labda Baada mwaka ngoja waje wanaojua watujuze

NB: ila mie sikopi Kwa kweli maana Kwa mahesabu ukikopa 10m nasikia ulipa pamoja na riba ambayo ni karibu sawa na Hela uliyokopa unaweza ulipe 20m
 
Siyo kweli kaka,hapo riba asilimia ngapi? Aliyekopa million 100 arudishe 200?!
 
Siyo kweli kaka,hapo riba asilimia ngapi? Aliyekopa million 100 arudishe 200?!
Sema ukweli unaoujua mkuu? ila amini nachokuambia nimefanya research za kimchongo nyingi sana🤣 kuhusu mshahara,makato sijui ya bima,Paye,psssf,Cwt na hayo ya kuhusu mkopo mkuu ila uhakika Zaid riba inazidi nusu ya Hela uliyokopa ukubali au ukatae
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wameona hauitumii ndo maana wmekupa
Hahahahaa, huo ni ukweli aisee.

Mimi nilikuwa nadaiwa Songesha, nilipoona maji yamezidi unga, nikaswitch to Halotel, nikaacha kuitumia Voda kuanzia kuweka vocha hadi M-pesa ikabaki tu online(kwenye simu), hapo ilikuwa mwaka 2020, wakawa wananidai kila mara, ilipofika mwaka 2021 wakaanza kuniambia wamenisamehe ila huo mtego sikunaswa.

Mwaka huu niliweka(nilitumiwa) hela M-pesa, nikajisemea hapa Songesha wanakula chao, bahati nzuri nikakuta kweli washanisamehe
 
Back
Top Bottom