Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ushauri kwa utumishi
Tenti ziwe angalau tatu kwa ajili ya kujikinga na jua au mvua. Wapande miti bila shaka miti inaota. Saili ziwe zinafanyika mapema Ili wa kurudi mikoani waweze kuondoka kurudi makwao.
Oral ya MDA tulikesha juani
Ukame ule na topographical mbaya kama Ile unapandaje miti pale..!!! kikubwa nachoona ili kutusaidia watafuta Ajira basi waongeze viti vya kuketi au mabenchi na turubai kiaina..
Nakumbuka Oral yangu nimeteseka sana na njaa maana pale wali kibakuli kidogo tu wanauza 4000-5000 so jobless wengi tunashinda na njaa. Pia niliteseka sana na jua ukicheck si wengine hizi rangi zetu. Ila nilivyoingia ndani kwa Jopo njaa yote ikapotea nikaanza kupambania job, Nikajitambulisha kwa history yangu Shortly na kusubiria maswali ya msingi ya taaluma yangu. But panel Ile ilikuwa peace tu yaan unapewa nafasi ya kufikiria point kama Iko mbali.
 
Pole sana prok, Nilivofika mara1 pale migiro nikahisi nimepotea[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kumbe ndo nimefika daah! Kile kibaridi cha hapo kisha likaja kufumuka jua nikajiuliza hivi ni wote huwa tunafanyia usaili hapa au ss tu tumeteuliwa [emoji3][emoji3][emoji3] nikasema lets keep it up kwakuwa kufika oral ni hatua kubwa sana
Ni hapo hapo yan. Mtihani kwa kweli[emoji23][emoji23]. Mimi hadi nywele zinapataga vumbi
 
Siku ndio imeisha hivyo tukiwa na agenda ya written TRA, kesho ni j4 siku ya placement. Subira na maombi viendelee
 
Ila hii jaman acha tu, mimi ile interview ya NAOT acha tu kilichonikuta. Asubuh kwanza nlikuwa nmempanga boda maana ninapokaa ni ndan kidogo, saa 11 nkaamka nkampigia akasema ashaamka anakuja, namaliza kuvaa nimpigie aje simu haiwaki, yaan haioneshi chochote. Nkajipa moyo atakuwa nje, natoka nje simuoni mtu yoyote, nlikaa kwanza nmepigwa na butwaa ishakuwa saa 12 na nusu. Ikabidi nitembeee hadi barabarani na suti yangu, ni mbali kidogo, nkapata boda, nikamwambia anikimbize awezavyo saa 1 kamili niwe Asha Rose Migiro. Boda alikimbia nlikuwa naona kifo hiki, tumefika na dk 5. Nkakuta washaanza kusoma. Nlikuwa na wasiwasi ntasomwa mapema tu halafu nianze kutoa macho. Kwenye ukaguzi sasa, msimamizi akakataa barua yangu ambayo interview zote nmekuwa nkitumia hiyo, akasema eti nmeaddress katibu muhtasi badala ya katibu, nkajitetea kuwa mimi kwa kweli kiswahili sielewi najua permanent Secretary ila kwa kiswahili sijui ni nan, akanambia umesoma mpaka law school hujui maana ya katibu muhtasi, et na boss akiona umemuaddress hivi atafurahishwa. Akanambia rudi ukaandikiwe barua mpya na iwe kutoka Dar. Nkamwambia sio kosa langu barua kaandika mtendaji wa mtaa kunitambulisha sio mimi, na kama ningeshajua ni kosa ningeshabadilisha maana muda wote nmekuwa nikitumia hii. Jaman dada akagoma kabisa. Wenzangu walikuwa wachache tu nane wakakaguliwa wote nikabaki mimi. Akanigomea kabisa. Nlililia, nlilia, yaan nlishindwa jizuia machoz yalikuwa yanaporomoka tu. Akawa ananipita tu. Baadae nkamfata tena akasema labda nikupeleke kwa boss wangu, nikaenda yule mama akaangalia ile barua akacheka, akasema kafanye tu oral mwanangu.
But since hapo nliharibiwa kabisa kisaikolojia. Yaan interview zote uwa nakuja huku kutoa feedback but ya NAOT kama mligundua nlibaki tu kimya. Yaan na maswali nikayaona magumu, acha tu. Ata nlivyorudi nyumbani nlijikuta tu nalia

Duh! Aisee Mkuu kwa mwendo huu, hawa watu inatakiwa wawe na hekima sana. Pole sana, yani nimeusoma ujumbe wako kama vile nilikuwepo eneo la tukio namna hiyo hali inaumiza.

Halafu kitu nilicho note ni kwamba mara nyingi hata kwenye Ofisi nyingine hawa watu wa chini huwa hawana hekima na sio waelewa kabisa, ni afadhali mtu akipatwa na tatizo adadisi ni yupi kiongozi wao kisha amface anaweza akapata msaada wa maana zaidi.

Sasa mtu anakwambia uende ukatafute barua upya na ni muda wa Oral, hivi ana akili kweli?
 
Kuna mdada ilikua written wote tumeingia ndani yeye kabakishwa nje anasumbuliwa kuhusu ID na kusimangwa juu amekuja ruhusiwa ndio tunapewa paper ila she was among wale ambao walikua shortlisted kwa Oral. Kwa ule mtihani aliopitia kama haikua muda wake asingetoboa. I believe muda ukifika hata vikwazo viwepo unatoboa.

Aiseeee haya mambo haya, hawa ndugu zetu sijui huwa hawawazi kama saikolojia ni kitu muhimu zaidi hata ya kujiandaa kwa kusoma sana.

Mtu anaweza akajiandaa vya kutosha, ila akisha tetereshwa kisaikolojia haya maswali anaweza asielewe yanataka nini.
 
HR TANZANIA INAWALETEA
TRA INTERVIEW QNS

1-10 multiple choices (10 marks)

11a.Differentiate btn International double taxation and domestic double taxation.
b.reasons for occurance of International double taxation.
c.mention two methods of double taxation

12a.Give similarities and differences between exempt VAT and zero rated vat.
b.conditions for a trader to be registered into VAT.
c.effects of VAT to a trader.

13a.Reasons for Tax disputes and measures to control them.

14.write down the procedures to solve the incidence of Tax disputes.

15.ilikua swali la kusolve duties/Tax liabilities za CIF.(25 marks)
Note,hii lilikua paper ya Tax management officer ii




Written ya TMO
1.Inclusion& exclusions in calculations tax
2.withholding tax
3.what is VAT,what one should have to be registered as VAT person
4.Dispute settlement
5.difrence btn zero rate and Exempt supply
6.Internationa Double Taxation
7.Calculations of import & export duties




1. Introduce your self
2. Differentiate tax base and tax administration
3. Wat is income tax
4. Wat is VAT
5. Functions of tax administration
6. Roles of taxation
7. Positive and negative impacts of digital economy




Naomben majibu ya haya maswali:


01:State penalties for making false or misleading statements under Tax administration Act Cap 438.


02:Explain causes and Effects of cancellation of VAT registration.


03:Explain methods that can be used to quantify the level of Tax Avoidance and tax evasion


04😀istinction and Similarities between identical and similar goods.



Qn no 3
Method of tax avoidance
1.transfer princing
2.Thin capitalization
3.Income capitalization
4. I ncome splitling
5.Income shattering



TAX EVASION METHOD
1 .Underdeclation of income
2.Overstating of expenses
3.Keeping two sets of accounts(moonlighting)
4. Smuggling


Taxation areas za kupitia...
1.Objectives of taxation.
2.Adam Smith canons of taxation.
3.Other canons of taxation.
4.X-tics of a good tax system.
5.6 steps of problem solving.
6.Classification of taxes.
7.Theories of equity in taxation.
8.Explain taxable capacity and factors affecting taxable capacity of a country.
9.Steps of problem identification.
10.Explain the TRA departments.
11.Explain taxes administered by TRA.
12.Explain tax compliance and the types of tax compliance.
13.How can we achieve maximum voluntary compliance?
14.Taxpayers obligations.
15.Problems associated with enforcement of taxpayers rights.
16.define tax evasion and tax avoidance and the causes of such acts.
17.Tax avoidance mechanisms.
18.How to minimize tax avoidance.
19.Consequences of tax evasion
20.Tax audit and its phases.
21.Tax base and the competing tax bases.
22.Sources of tax laws.
23.Basic principles construing tax statues.
24.Elements of tax.
25.Factors on which the ultimate burden of tax depends on.
26.x-tics of a broad tax system.
27.Tax planning techniques.
28.Research process.
29.Self assessment and the advantages of self assessment.
30.Categories for which taxes may be levied.
31.Procedures for gathering tax audit information.
32. Common criteria that satisfy the scientific scientific research.
33.significance of classifying a person as resident person.
34.Differentiate between tax impact and tax incidence.
35.Meaning of employment and the difference between contact of service and contact for service.
36.Tax Regulations that are used in tax laws
37.Main tax laws


CC
Unknown Source

Wahusika iishi humo
 
Kwanza siku tunaenda written, mimi nmezoea kutoka kule home na bado since mitihan uwa ni saa moja, sasa wa Naot ilikuwa saa 6. Nkaona tu ntapanda daladala maana muda upo. Kwanza pale sabasaba hii ndo ilikuwa mwanzo kushuhudia, yaani watu wanajaa hadi wanasimama ndo daladala nyingine inapakia, tukasubirii baadae ndo tukapanga km nusu saa hiv, hapo naona tushachelewa. Basi nlipanda daladala nkaweka mkono nje, daladala nyingine ikapita kabisa pemben ikanibana mkono nlipiga kelele, ikaniachia mstari hadi nyama ya ndan ikaonekana, na ikanichubua ngoz ile nguo ya mikono mirefu nilivaa, aisee, nmefika na maumivu makali, tukasubirishwa tena, tukaja fanya ntihan saa 8 sijui 9. Mkono unaniuma sio poa na hapo nmeuficha kwenye nguo yangu. Yaan sasa hivi nkisikia NAOT moyo unapiga paa, nawaza maswahibu niliyopitia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Namuwaza huyo dada, yaan bora ata mtu anikumbushe MDA na LGAs sio NAOT

Duh! Watu mumepitia mengi sana.

Hahahaha! Mkuu vipi mkeka wa NAOT ukitoka umefanikiwa, utaenda?
 
Huwezi kujiamini kwa kitu ambacho aliyekufanyia usaili sio ndugu yako Wala hauna mahusiano nae.Kikubwa tu Wakati wako Ukifika kama Mungu Kaamua basi kazi itakuwa yako tu hata ushindani uwe vipi.Kikubwa tupende kushukuru Mungu Kwa kila jambo liwe Baya au zuri tulipokee.

Ni kweli sana Boss, asante kwa kutukumbusha.
 
Kuna jamaa wa utumishi aliniambia "Hivi umesoma una degree kweli wewe "? Siku ya written. Moyo uliniumaaaaa,nikapotezea nikapiga mtihani nikarudi zangu Tandahimba. Pamoja na kuniambia vile matokeo oral yakatoka nikaitwa nikaenda Asha Rose Migiro nikapiga oral nipo nasubiri placement.Nikipata asante Mungu nikikosa asante Mungu ila nitaendelea kuomba na kupambana.

Hahahaha! Japo sio mazuri lakini hilo swali linachekesha sana endapo mtu una simuliwa kama hivi.

Ila kwa liliyekukuta inauma kupitiliza.
 
Umenikumbusha huu mkeka uliondoka na mwanangu kimasihara.
Jamaa yangu alikuwaga hana imani kbs kuwa kuna kutoboa psrs, baada ya kuona ss tunaaply na yeye akaaply TRA, KUMBUKA lengo lake kubwa lilikuwa kuja kutest wanatoaje pepa, wanasahihishaje, ili ajipange sasa kwa saili zijazo. Akapiga written kawaida tu akaona hapo hatoboi akajua sasa maswali wanatoaje akarudi home kula msuli heavy, matokeo yanakuja kutoka ya ORAL YUMO [emoji3][emoji3][emoji3] HALAFU KUMBUKA KASHAKULA MSULI MZITO WA SAILI ZIJAZO. kwahiyo jamaa akaenda kupiga oral kiulaini sana kwasababu alikuwa anajinoa na kweli akapata kazi.
Nikajifunza zaidi huku PSRS NI KAZI NA kazi ni Ridhiki na Mtoaji ni Mungu WAKATI WETU UKIFIKA NARUDIA TENA WAKATI WETU UKIFIKA HAKUNA WAKUPINGA NA HATUTATUMIA NGUVU KUBWA SANA, kwahiyo tusiache kuomba, tusiache kuthubutu Ni suala la muda tu. PSRS hakuna cha ugenius wala ujuaji ni suala la muda tu kwasababu tunatafuta ridhiki ambazo ndio kazi zenyewe na Mpaji ni Mungu.

Duh! Aiseee Mkuu hii simulizi ni motivation kubwa kwa ambao wanahisi kukata tamaa.

Yaani wakati wako ukifika hata mwenyewe unaweza usielewe imekuwaje kuwaje lakini ndio hivyo unafanikiwa.
 
Ule mkeka 98% walioingia oral walipata kazi. Nakumbuka sana aisee nilipata 49.0 kwenye written na jamaa zangu wote waliotoboa written wamelamba utamu wa asali.

Aisee hii kitu inaumiza, unakuta ni watu ulikuwa unajiandaa nao na wengine unawaona kabisa hawakuwa serious lakini ndio hivyo wamepita na wewe umebaki.

Muda wako utafika Mkuu, endelea na mapambano.
 
Kuna machoko wanajiona Miungu watu sana ,kauli chafu chafu za kashfa na shombo ndio maisha yao , ulimbukeni ni tatizo sana kwa watanzania .
Hata huku uraiani tabia ni hiyo hiyo .
 
Back
Top Bottom