Ndugu yangu uko sahihi sana. Kuna mdada alitoka kwenye usaili fulani na kurudi nyumbani akila siku nzima kwa makadirio ya haraka iliisha wiki hayuko sawa.
Sababu ni kwamba kuna maneno ya kukatisha tamaa aliambiwa na moja ya wanapannel kwenye Oral, yakamtoa kwenye reli kabisa akawa na kigugumizi kuanzia hapo akiulizwa maswali yanayofuata akawa anajibu kisha anazidiwa na kulia.
Kwa hiyo alivyotoka kwenye mtihani akawa anaumia kwamba tayari amefeli, hata kumpa moyo ni ngumu kwa sababu hoja yake ni atafaulu vipi wakati maswali mengi hajayajibu!
Mkeka ulipotoka jina lake likawepo na kuna baadhi ya waliotoka kwa kujiamini na kuanza kumfariji majina yao hayakuwepo.
Nadhani jamaa wa panel labda waligundua kuna kuna mahala waliteleza kwa hiyo wakaona waangalie namna ya kumfidia kibinadamu.
Ni ule mkeka wa TRA wa mwaka huu uliowapa watu wengi ajira.