Ila hii jaman acha tu, mimi ile interview ya NAOT acha tu kilichonikuta. Asubuh kwanza nlikuwa nmempanga boda maana ninapokaa ni ndan kidogo, saa 11 nkaamka nkampigia akasema ashaamka anakuja, namaliza kuvaa nimpigie aje simu haiwaki, yaan haioneshi chochote. Nkajipa moyo atakuwa nje, natoka nje simuoni mtu yoyote, nlikaa kwanza nmepigwa na butwaa ishakuwa saa 12 na nusu. Ikabidi nitembeee hadi barabarani na suti yangu, ni mbali kidogo, nkapata boda, nikamwambia anikimbize awezavyo saa 1 kamili niwe Asha Rose Migiro. Boda alikimbia nlikuwa naona kifo hiki, tumefika na dk 5. Nkakuta washaanza kusoma. Nlikuwa na wasiwasi ntasomwa mapema tu halafu nianze kutoa macho. Kwenye ukaguzi sasa, msimamizi akakataa barua yangu ambayo interview zote nmekuwa nkitumia hiyo, akasema eti nmeaddress katibu muhtasi badala ya katibu, nkajitetea kuwa mimi kwa kweli kiswahili sielewi najua permanent Secretary ila kwa kiswahili sijui ni nan, akanambia umesoma mpaka law school hujui maana ya katibu muhtasi, et na boss akiona umemuaddress hivi atafurahishwa. Akanambia rudi ukaandikiwe barua mpya na iwe kutoka Dar. Nkamwambia sio kosa langu barua kaandika mtendaji wa mtaa kunitambulisha sio mimi, na kama ningeshajua ni kosa ningeshabadilisha maana muda wote nmekuwa nikitumia hii. Jaman dada akagoma kabisa. Wenzangu walikuwa wachache tu nane wakakaguliwa wote nikabaki mimi. Akanigomea kabisa. Nlililia, nlilia, yaan nlishindwa jizuia machoz yalikuwa yanaporomoka tu. Akawa ananipita tu. Baadae nkamfata tena akasema labda nikupeleke kwa boss wangu, nikaenda yule mama akaangalia ile barua akacheka, akasema kafanye tu oral mwanangu.
But since hapo nliharibiwa kabisa kisaikolojia. Yaan interview zote uwa nakuja huku kutoa feedback but ya NAOT kama mligundua nlibaki tu kimya. Yaan na maswali nikayaona magumu, acha tu. Ata nlivyorudi nyumbani nlijikuta tu nalia