Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ndugu zangu mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mungu wetu yu hai hata leo. Baada ya ujobless kwa miaka 7, sasa ameniona kupitia utumishi. Nawasihi waliokosa kutokata tamaa, nafasi yao ipo. Nimefanya Oral moja tu, nimechaguliwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mjuzi, tumtegemee yeye. Kutoka familia duni, bila connection, amenifanyia wepesi na upendeleo mkubwa sana.

NB: Status yangu (Selected for null kwenye app na Selected for Oral kwenye website)
Hongera sana mkuu, kila la kheri na ukawe mtumishi mwema
 
Ila hii jaman acha tu, mimi ile interview ya NAOT acha tu kilichonikuta. Asubuh kwanza nlikuwa nmempanga boda maana ninapokaa ni ndan kidogo, saa 11 nkaamka nkampigia akasema ashaamka anakuja, namaliza kuvaa nimpigie aje simu haiwaki, yaan haioneshi chochote. Nkajipa moyo atakuwa nje, natoka nje simuoni mtu yoyote, nlikaa kwanza nmepigwa na butwaa ishakuwa saa 12 na nusu. Ikabidi nitembeee hadi barabarani na suti yangu, ni mbali kidogo, nkapata boda, nikamwambia anikimbize awezavyo saa 1 kamili niwe Asha Rose Migiro. Boda alikimbia nlikuwa naona kifo hiki, tumefika na dk 5. Nkakuta washaanza kusoma. Nlikuwa na wasiwasi ntasomwa mapema tu halafu nianze kutoa macho. Kwenye ukaguzi sasa, msimamizi akakataa barua yangu ambayo interview zote nmekuwa nkitumia hiyo, akasema eti nmeaddress katibu muhtasi badala ya katibu, nkajitetea kuwa mimi kwa kweli kiswahili sielewi najua permanent Secretary ila kwa kiswahili sijui ni nan, akanambia umesoma mpaka law school hujui maana ya katibu muhtasi, et na boss akiona umemuaddress hivi atafurahishwa. Akanambia rudi ukaandikiwe barua mpya na iwe kutoka Dar. Nkamwambia sio kosa langu barua kaandika mtendaji wa mtaa kunitambulisha sio mimi, na kama ningeshajua ni kosa ningeshabadilisha maana muda wote nmekuwa nikitumia hii. Jaman dada akagoma kabisa. Wenzangu walikuwa wachache tu nane wakakaguliwa wote nikabaki mimi. Akanigomea kabisa. Nlililia, nlilia, yaan nlishindwa jizuia machoz yalikuwa yanaporomoka tu. Akawa ananipita tu. Baadae nkamfata tena akasema labda nikupeleke kwa boss wangu, nikaenda yule mama akaangalia ile barua akacheka, akasema kafanye tu oral mwanangu.
But since hapo nliharibiwa kabisa kisaikolojia. Yaan interview zote uwa nakuja huku kutoa feedback but ya NAOT kama mligundua nlibaki tu kimya. Yaan na maswali nikayaona magumu, acha tu. Ata nlivyorudi nyumbani nlijikuta tu nalia
Barua ya mtendaji??? Hua mkifika oral ndo mnaambiwa mwende na barua ama???
 
Ina maana jamaa yako alikuwa anapiga msuli heavy bila hata kuwa na tangazo la kazi.

Na hapo juu umesema alijua hatatoboa, sasa msuli heavy ulikuwa wa nn, kumbuka kusoma bila kuwa na events yoyote vitu huwa vina evaporate.
Sio tu kuevaporate,yan alikua anasoma kwa vacancy ipi mana position hutofautiana
 
Ukame ule na topographical mbaya kama Ile unapandaje miti pale..!!! kikubwa nachoona ili kutusaidia watafuta Ajira basi waongeze viti vya kuketi au mabenchi na turubai kiaina..
Nakumbuka Oral yangu nimeteseka sana na njaa maana pale wali kibakuli kidogo tu wanauza 4000-5000 so jobless wengi tunashinda na njaa. Pia niliteseka sana na jua ukicheck si wengine hizi rangi zetu. Ila nilivyoingia ndani kwa Jopo njaa yote ikapotea nikaanza kupambania job, Nikajitambulisha kwa history yangu Shortly na kusubiria maswali ya msingi ya taaluma yangu. But panel Ile ilikuwa peace tu yaan unapewa nafasi ya kufikiria point kama Iko mbali.
Duh nkifanikiwa oral ntabeba msosi kabisa bas kama mambo yenyew ndo hvo[emoji1787]
 
kwema kabisa,bado nasubiria mkando wangu maana matumaini 0
Kuwa strong sio wew tu hio hali maana wengine tulivyoingia tu kwenye panel tukapoteza fahamu nakuja kuzinduka nakabidhiwa vyeti na kuelekezwa pa kupitia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] lkn nina bonge la tumaini kwenye pdf na huenda ukawa unahofia na wenzio hivohivo hawaelewi wamefanya nn, jipe moyo na aamini huku ukielekeza maombi na kusonga mbele kwa kila fursa ijayo. Siku yetu ikifika haipingwi hata ujibuje. When God say Yes no body can say No!


#Waiting for miracles

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hello guys. Kwa wakazi wa Moshi/Arusha kuna usafiri private kwa watu wanne interested.
Bei ni Tshs elfu 65 tu Go and return.
Tutaondoka jumamosi tarehe 17/12/2022 saa moja asubuhi.
PACKAGE INCLUDES:
1.Usafiri kutoka Moshi bus stand saa moja asubuhi ya tarehe 17 hadi Dodoma mjini.
2. Usafiri kutoka Dodoma mjini hadi UDOM ukumbi wa CIVE au kumbi jirani tarehe 18 saa kumi na mbili asubuhi (ili kuwahi interview).
3. Usafiri kutoka ukumbi wa interview hadi Dodoma mjini tutakapofikia.
4. Baada ya interview usafiri hadi Moshi stand. Siku ya tarehe 19 saa moja asubuhi.
✓Other benefits include:
•Kudiscuss kwenye gari kwa pamoja
•Kusimama popote njiani and other benefits of a private travel.
DM if interested.
N.B HUU NI MSIMU WA SIKUKUU, UNAWEZA UKAKWAMA EITHER KWENYE GARI ZA ABIRIA KWENDA AU KURUDI, AU NAULI KUPANDA KUPITA KIASI.
MALIPO YANAPOKELEWA KWA MKONO MWISHO SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 16/12/2022 SAA SITA MCHANA
 
Back
Top Bottom