Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Intro ya tangazo mara nyingi huwa wanaikopi na kupaste wanaedit kidogo tu kama tarehe.

Nimejaribu kupick random majina ya walioitwa kazini na kwenda kuangalia kwenye tangazo la mkando, nimewakuta wote kwenye tangazo niliowapick random. Kwa mantiki hiyo wanaweza wasiwepo kabisa kutoka database.

Ambao huwa wanatoka database kihalali ni ambapo tangazo litasema hivyo bila kutaja tarehe ya oral.
wapo, watu wa Tengeru, IMF nk walishaitwa kitambo hao walio kwenye PDF ni kutoka kwenye kanzidata
 
Nikifanikiwa kuupata mrija wa asali nataka nikutane na Mwifwa

Nlishakataga tamaa hata ya kuapply,ila ye ameupa hype sana huu uzi nkasema why not em ngoja nijarbu tena.

So wacha tuone,nipo nasubiri kua shortlisted LGA

Kuwa shortlisted ni uhakika kama ulifata vigezo katika kuomba hyo nafasi.

Suala la muhimu ni wewe kuanza maandalizi mapema, tambua kuwa PSRS huwa wanatoa muda mfupi ambao mara nyingi si zaid ya wiki 1 tangu kutoa tangazo hadi tarehe ya usaili wa kuandika.
 
Mwifwa na wengineo,mmefanya huu uzi kuwa mtamu sana.Yani hakuna siku vijana wote waliokandwa au wanaokandwa watashindwa kuingia humu kujifariji kidogo.Tuendelee kumuomba Mungu na tuiombee Serikali yetu iendelee kutoa Ajira kwa wingi.
Pongezi kwao
Sekretarieti ya Ajira kwa kuendesha michakato hii ya Ajira,hakika ni raha Sana kuona vijana wenzetu tunaowafahamu wamepata Ajira,inatia matumaini sana ya Kuwa nasi Wakati wetu ukifika basi Tutapata.
Mungu ni wetu Sote.Tuendelee kupambana na kumtanguliza yeye vijana wenzangu.
Ahsante sana mkuu, tuishi humu hadi kieleweke
 
Nipe muongozo wataalamu wa ajira portal

Vyeti vya upload ni lazima viwe na muhuri wa mwanasheria au mahakama au la!?

Na pale verification certificate ndi Nini !?

Naomba muongozo mzee Mimi[emoji1]

Bila shaka ushapata muongozo.

Kama bado: Ni lazima vyeti viwe na muhuri wa Mwanasheria/Wakili/Hakimu.

Kwenye sehemu ya Verification inawahusu waliosoma nje ya Nchi ambapo vyeti vyao huwa vinahakikiwa na TCU
 
wapo, watu wa Tengeru, IMF nk walishaitwa kitambo hao walio kwenye PDF ni kutoka kwenye kanzidata
Sawa mkuu, sikuhakiki hao, nilihakiki kwa wanasheria wa OSG ingawa pdf ishaondolewa na haijarudishwa hadi sasa
 
Kwahiyo wanaweza kufuata barua? Isije ikawa wameanza kuipika mpya hiyo pdf
hata mimi sielewi kwanini wameondoa, niliipakua hii before hawajaondoa ila nahisi may be wanaongeza taasisi au wanabadilisha kitu ndipo waapload tena
 
Bila shaka ushapata muongozo.

Kama bado: Ni lazima vyeti viwe na muhuri wa Mwanasheria/Wakili/Hakimu.

Kwenye sehemu ya Verification inawahusu waliosoma nje ya Nchi ambapo vyeti vyao huwa vinahakikiwa na TCU
Nashukuru kwa muongozo
 
Najaribu kuwaza incidence ambayo jina uliliona kabla hawajafuta ila baada ya marekebisho hulioni.....ha ha ha...hapo itabidi uende hivyo hivyo kufata barua na tangazo la awali.
Oohoo hapo utapoteza nauli yako yani ni bora ukawapigia simu kwanza maana kunajamaa angu waliitwa kuchukua barua kwenye post iliyohitaji watu watatu ila kwenye list ya placement waliongezwa na yeye alikua mmojawapo ya walioongezwa kwenye list, alipofika akaambiwa ni makosa yalijitokeza post ilihitaji watatu tu walioongezwa hawana barua
 
Back
Top Bottom