Mwifwa na wengineo,mmefanya huu uzi kuwa mtamu sana.Yani hakuna siku vijana wote waliokandwa au wanaokandwa watashindwa kuingia humu kujifariji kidogo.Tuendelee kumuomba Mungu na tuiombee Serikali yetu iendelee kutoa Ajira kwa wingi.
Pongezi kwao
Sekretarieti ya Ajira kwa kuendesha michakato hii ya Ajira,hakika ni raha Sana kuona vijana wenzetu tunaowafahamu wamepata Ajira,inatia matumaini sana ya Kuwa nasi Wakati wetu ukifika basi Tutapata.
Mungu ni wetu Sote.Tuendelee kupambana na kumtanguliza yeye vijana wenzangu.