Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mimi toka jana naugulia maumivu ya kukandwa nikashindwa hata kuwapongeza waliopata......sijaamini bado kuwa nimekosa nafasi zile za NPS. Ha ha ha. Written nilifanya fresh kabisa, na huko oral sijui nini kilibadilika...

Anyway ndiyo life hilo...maisha lazima yaendelee. Hongereni mliopata mrija wa asali. Jina la Mungu lipewe sifa.
Usikate tamaa hakika ipo siku utafanikiwa
 
Habari za leo Wakuu.
Jana niliahidi kuleta mrejesho.
Nilifanya written Interview nane ,saba zote sikufika hata oral zote nilikuwa napata namba za viatu , yanane nikafika oral na ndo hii niliyopata placement.


Nilingia kwenye chumba cha wakandaji nikiwa nimevaa kadeti, shati na koti langu vizuri kabisa. Nilipoingia tu ndani nikawasalimia wakandaji wakaitikia then mmoja akasema karibu kiti.




Nilitumia muda mfupi sana nimetoka wadau wanashangaa mbona mapema sana nadhani walijua nimefukuzwa mle ndani😂😂
Baada ya hapo nilijiona mjinga sana maana nimeshindwa kujibu swali moja. Hamu ya kula ilikata kabisa niliona kama nimepoteza nafasi lakin Mungu ndo alijua.
Nimejifunza ili ufanikiwe lazima upite mambo magumu( Rejea wimbo wa Christina Shusho-Dhahabu)

1. Usikate tamaa jipe moyo ipo siku utatoboa bahati huwapata wale wanaojaribu.
2. Ukiitwa kwenye usaili fanya maandalizi haswa. Piga msuli yatima haswa pitia job descriptions zifuatilie moja baada ya nyingine. Saili nyingi za nyuma nilikuwa sijindai vizuri pia nilikuwa sifuatili trends za maswali. Unakuta unasoma research kumbe wameshaacha kutoa research.
3. Omba Mungu yeye ndo anajua ni lini atakupa.
4. Usibanduke kwenye huu Uzi. Jamii forums ni kila kitu imagine nimeanza kufuatilia huu uzi mwezi wa 10 nikapata hints kibao nikafufua matumani , mwezi wa 10 huo huo nikatoboa oral kwa mara ya kwanza. Hata uwe kipanga au kenge namna gani bila kujua trends na namna ya kujibu maswali kutoboa ningumu.

Natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote wa uzi huu (Mwifa, Wizy a.k.a Wkingz mzee wa status😂😂 na wengine wote) kwa michango yenu .

N.B: Mtoto wa masikini kabisa ametoboa bila connection acha kulalamika inawezekana.
Nilivyofurahi mimi wife amefurahi mara 10 yake🤣🤣🤣
Hongera sana mkuu, Mungu mwema
 
Ahsante sana mkuu. Muda ndio huwa unadetermine mambo, kwa sasa hilo haliwezekani ukizingatia mfumo wa ajira tuliorisishwa na Mzee wa Chattle pia unapigilia msumari.

Binafsi nipo kwenye early 30, mfumo usingetikiswa ningeingia kwenye mrija nikiwa kwenye late 20.

This is all about God's plan, tunapaswa kushukuru pia
Hongera sana mkuu, mnazidi kutupa matumaini na sisi ambao tulikuwa tumekata Tamaa.
 
Hata kama ni kwenye database walitakiwa kutangazwa na kuwekwa kwenye PDF Moja na sio kimagumashi
Kuna rafiki angu tulifanya wote usaili MDA, Sa kabla ata placement za MDA hazijatoka akapata kazi legal officer halmashauri fulan, na hajawi fanya interview yoyote tofauti na hizi, na hiyo placement ilitoka nahisi December mwanzoni.
 
Finally I made it!

Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion

Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.

Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.

Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.

PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.

Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.

Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.

Join me in celebrating this remarkable history!!
Hongera sana kaka...
 
Back
Top Bottom