Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ndio hivyo mkuu.

Sikuwahi kujisumbua kuangalia status baada ya Oral hadi siku placement ilipotoka ndio nikaangalia nikakuta imeandikwa SELECTED FOR ORAL INTERVIEW, pia ile namba ya written ikawa bado inaonekana pale.
iyo ni kwenye web. je kwenye application yao iliandikaje?
 
Habari za leo Wakuu.
Jana niliahidi kuleta mrejesho.
Nilifanya written Interview nane ,saba zote sikufika hata oral zote nilikuwa napata namba za viatu , yanane nikafika oral na ndo hii niliyopata placement.


Nilingia kwenye chumba cha wakandaji nikiwa nimevaa kadeti, shati na koti langu vizuri kabisa. Nilipoingia tu ndani nikawasalimia wakandaji wakaitikia then mmoja akasema karibu kiti.




Nilitumia muda mfupi sana nimetoka wadau wanashangaa mbona mapema sana nadhani walijua nimefukuzwa mle ndani😂😂
Baada ya hapo nilijiona mjinga sana maana nimeshindwa kujibu swali moja. Hamu ya kula ilikata kabisa niliona kama nimepoteza nafasi lakin Mungu ndo alijua.
Nimejifunza ili ufanikiwe lazima upite mambo magumu( Rejea wimbo wa Christina Shusho-Dhahabu)

1. Usikate tamaa jipe moyo ipo siku utatoboa bahati huwapata wale wanaojaribu.
2. Ukiitwa kwenye usaili fanya maandalizi haswa. Piga msuli yatima haswa pitia job descriptions zifuatilie moja baada ya nyingine. Saili nyingi za nyuma nilikuwa sijindai vizuri pia nilikuwa sifuatili trends za maswali. Unakuta unasoma research kumbe wameshaacha kutoa research.
3. Omba Mungu yeye ndo anajua ni lini atakupa.
4. Usibanduke kwenye huu Uzi. Jamii forums ni kila kitu imagine nimeanza kufuatilia huu uzi mwezi wa 10 nikapata hints kibao nikafufua matumani , mwezi wa 10 huo huo nikatoboa oral kwa mara ya kwanza. Hata uwe kipanga au kenge namna gani bila kujua trends na namna ya kujibu maswali kutoboa ningumu.

Natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote wa uzi huu (Mwifa, Wizy a.k.a Wkingz mzee wa status😂😂 na wengine wote) kwa michango yenu .

N.B: Mtoto wa masikini kabisa ametoboa bila connection acha kulalamika inawezekana.
Nilivyofurahi mimi wife amefurahi mara 10 yake🤣🤣🤣
Hongera brother
 
Wao wanatakiwa wawe na barua ya mwajiri sio kwmba hawaruhusiwi kuomba kz inservice kibao tunafnya nao usaili
Hii ya Kusema kibao ni uongo..
Me naamini in-service ambao wanaomba kazi psrs Huwa wako tu interested na taasisi husika au kufuata maslahi kimtindo.. Sasa ukija kwenye Uhalisia hizo taasisi zenye maslahi ni Chache sana na nadra kutangaza hizo kazi sasa hao in-service kibao wanatoka wapi..?

Pia, in-service wanaomba kazi psrs ni hawa vijana ambao hawana hata miaka 5 kwenye kazi zao(utumishi wa Umma) hawa ndio wasumbufu, ni ngumu sana kukuta senior worker Yuko huko Halmashauri ameridhika na majukumu yake, Mishe zake na yuko na familia kubwa akawa anahangaika namna hyo.
 
Good things happen when you least expect them.

Mifano mnayo humu wale wenye makeke sana wali disappear kama diffusion ya ushuzi, na wale humble wapo kupongezwa humu. Amini kama ulifanya vizuri basi you deserve it and it will happen to you no need to tail it every second.
 
Back
Top Bottom