Hapa mkuu umenichanganya kidogo kwa huo mfano wako na jamaa yako, umekaa kama ulikuwa ni sehem ya panel, hofu yangu tu ni wengine humu kuhisi huyo jamaa yako ni wewe.
Hilo swali kw hakika linataka tu kujitambulisha majina yako, kama yanavyoonekana katika hivyo vyeti. Pili, kwenda moja kwa moja kueleza kuhusu elimu yako, kwa kutaja Institution/school ulisoma/ulisomea miaka uliyosoma hapo, na ulipata award/uli-achieve nini.
Mfano;
Kwa majina naitwa .....
Ningependa kuelezea kuhusu elimu yangu na mafanikio niliyoyapa kama ifuatavyo;
2014 - 2017 nilikua chuo x, nikisomea shahada/stashahada ya uinjinia , na kufanikiwa kupata shahada/stashahada ya uinjinia.
2012 - 2014 nilikua shule ya sekondari flan, nikisoma masomo ya advanced secondary na kufanikiwa kupata Advanced Certificate of secondary education.
2008 - 2011 nilikua shule ya sekondary fulani, nikisoma masomo ya secondary na kufanikiwa kupata Certificate of secondary education.
Nafikiri kuna ma-hr humu wanaweza nirekebisha na kunisahihisha.