Kuna kitu nahitaji kuuliza yeyote mwenye wazo au experience kuhusiana na hiki naomba anipe jibu, kati ya kuajiriwa au kujiajiri ni kipi kinamfaa mtu ambaye anapenda kusafiri yani yeye malengo yake ni kutafuta hela ili asafiri na kutalii tu nchi mbalimbali duniani kila mwaka, hana familia wala mtegemezi yeyote yule yani hela yake anayopata ni ya kutumia yeye na kusaidia wenye shida apatapo nafasi
Kwenye kuajiriwa inajulikana kwamba kila mwaka lazima kuna likizo ya mwezi kwa kila mtumishi ila kwenye kujiajiri ndio haijulikani atapata lini muda wa kusafiri, ikiwa biashara yake itahitaji uwepo wake kila siku maana nature ya biashara nyingi za kibongo hadi zije kusimama zenyewe kwa kuweka tu watu bila kuhitaji uwepo wako kila siku, basi itachukua muda mrefu kwahiyo malengo ya kusafiri nje kila mwaka atachelewa sana kuyatimiza
Ndio nimeona nililete kwenu wadau since huu uzi unahusiana na mambo ya ajira, yeyote mwenye maoni au ushauri juu ya mtu wa aina hiyo ni kipi kitamfaa kati ya kazi au biashara, natanguliza shukrani