Mkuu usijali, Kama ulifanya Oral Mungu atatenda miujiza kikubwa usikate tamaa na usipoteze imani kwake... Kila kitu kinawezekana...
Mimi nakumbuka nilianzaga kufanya interview 2021 ya TRC interview yangu ya kwanza nilipata 58, wakanikanda walichukua kuanzia 60. Ilikuwa ya System Administrator.... Niliumia sana kwa sababu aim ya kwenda kufanya haikuwa kufauru na kupata kazi balu kujifunza , sasa zile marks zili ni impress wangenichagua nikaenda practical nijue najifunza nini tena practical.
But sikukata tamaa, but sisi course zetu watu wa IT hazitoki nafasi mara kwa mara ni mara chache sana so ikikupita unaweza subira hata miezi 6 tena. Inshort watu wa IT kwa mwaka kafanya sanaaa interview ni tatu.... Hata range yetu ya kupata placement sio kubwa.... Unaweza kuta mwaka uliopita watu wa Tehama kuchukuliwa hawazidi 50.
Basi kama sikosei hiyo TRC , ilikuwa mwezi wa kwanza au wapili mwishoni.. nikakaaa miezi mingi takribani miezi sita ila nafasi zilikuwa zinatoka but ubaya yani IT ni kubwa.... Kuna networking, administrator , database, security, web developer ,programmer etc....
Sasa unatakiwa uwe umejitune unapoona unapaweza ukienda tu kila interview unakuwa unapoteza hela zako, cz mfano mimi najijua kabisa hapo Database siwezi kivile kwenda kubahatisha, so inabidi usubilie kile unachoweza ndio tangazo litoke ndio uende, but kuna watu wanajiweza wao zote twende.
Basi bwana ,mimi nikachagua za kufanya so nikawa nachukua material, pamoja na video tutorial huku nikajiunga group la watafutaji la utumishi, so watu wakienda wanashare leo maswali yalikuwa hivi ....basi ukiona hiyo topic naenda nasoma kidogo kidogo na practice hivyo yani....
Basi bwana:...... Kusoma ikawa daily routine yangu, sio kila siku but nikipata muda nasoma yani haiwezi pita week 2, sio kusoma ile serious viileeee ...no sometimes upo kitandani unacheck video tutorial na notes au una solve maswali hivyoooo... Mara unaingia website za maswali na majibu ili mradi kichwa kisipoe kikasahau...., Nilikuwa nasoma any useful material ambayo nilikuwa naona yanaweza nisaidia...
Pia nikawa nimenunua note book, pale mbele nikaweka target kuwa nikienda interview yoyote basi written nisishuke 75% ...practical pia niliweka nakumbuka na oral niliweka tu pass ...
So maisha yakawa yanendelea huku experience nyengine napata humu, kwenye hili jukwaaa.... Mimi hadi kujibu oral nilichukua humu technique kuna mtu aliwahi andika humu .... Hasa lile swali la Education background / tell us about yourself ....
So nikaendelea ,huku nasubiria tangazo la kazi litokeee.... Pia nilikuwa naombaga na private but kule ilikuwa kama tu nikipata nijishikize but my dream was serikalini kwa sababu ya Security pia nilikuwa naimani Carrier yangu itakuwa haraka sana....
Nakumbuka mpka mwaka 2021 unaisha hazikutoka kazi tena za system administrator baada ya zile za TRC ...tukaingia 2022........Itaendeleeaaaa
Nb: Watu wa tehama mnaweza chukua experience mkajaribu kupractice....