Hakuna kitu chochote cha ajabu ambacho jobless anapitia. Mchakato wa ajira ni process inayoinvolve players wengi. Na tatizo haliwezi kuwa mtu mmoja bali mfumo mzima ulivyo.
We all have been there. Zamu yako itafika na kama Mungu amekuandikia hiyo kazi utaipata wala hakuna shaka juu ya hilo. Zamu yako ikifika hakuna wa kuzuia.
Mwaka 2019, nilifanya interview moja tu na ya kwanza ya PSRS na nikalamba asali right away. Mdogo wangu Mwifa amefanya interview nyingi hadi kuja kulamba asali. Lakini leo wote tumesahau na kila mtu anaendelea na maisha.
Usikate tamaa ukakufuru hadi kuanza kuwatakia wenzio mabaya, utakimbiza baraka zako. Katibu sio tatizo. Kwa uzoefu wangu, ukitaka kupata ajira serikalini fanya yafuatayo.
Muamini Mungu. Yani kuwa na imani kwamba kuna higher being mwenye nguvu kuliko wewe na mwenye uwezo wa kukusukumia mambo yako yakaenda.
Fanya maandalizi ya maana. Soma sana kada yako. Kifupi imaster taaluma yako ili popote watakapokuleta usiwe na shida
Omba kazi zote na attend saili zote uongeze possibility ya kupata hiyo kazi. Inabidi uwe smart kwa ujumla
Wakati unasubiri michakato ya ajira ya serikali, unaeza pia anza kuangalia michakato mingine ya private sector au ajira binafsi na ujasiriamali mdogo mdogo ili usiwe idle ukawa na pressure kubwa ya kusubiri matokeo