Nilikua private kuanzia namaliza chuo. Lakini changamoto ni kwamba kwa kampuni na post niliyoishika ilikua nategemea mshahara kwa 100%.
Watoto, mke, wazazi na mimi mwenyewe ule mshahara ulikua hautoshi. Nipo kwenye kampuni kwa zaidi ya miaka miwili nikaamua nikasome ili sasa ama mshahara upande au niweze omba post zitakazoanza kulipa 2M kama takehome.
Nikajibiwa sisi tunajua tumemuajiri mtu aliyemaliza masomo hayo ya kutaka kwenda kusoma kampuni haisapoti. Mwaka Jana nilitaka kukopa 2M kwenye taasisi za fedha, siyo pesa nyingi kiasi hicho ule mlolongo niliokumbana nao wa ama gari au hati na pamoja na yote inabidi HR atie neno.
Nikafikiria nikaona nipambane na utumishi. Mungu mkubwa nikatoboa, washkaji zangu wakanicheka kwakua we all know nakuja kupokea peanuts huku lakini naamini in a long run kuna kitu nitafanya.