Kwanini uwanja ulilipuka kwa shangwe alipotambulishwa Samia Kama 'iron lady'?

Kwanini uwanja ulilipuka kwa shangwe alipotambulishwa Samia Kama 'iron lady'?

Chawa bana, mnadhani hatukuona hilo tukio? Kila kiongozi alipigiwa makofi kivyake, hakuna rais yoyote aliyepigiwa makofi ya tofauti mpaka ulete hizi propaganda za kijinga.
Punguza makasiriko mkuu, SAMIA ndio Rais wako Hadi 2030
 
moja, alikuwa mwsnamke pekee mkuu wa nchi
Na mwanamke ameumbwa kupendwa na kupewa attention na Rutto inaonekana analijuwa hili vyema.

Mama Jana kalala unono sana Kwa attention ile na kupewa fursa ya kutowa hotuba fupi.
 
Kumbe mama Samia sio wa mchezo mchezo.
Uwanja ulilipuka kwa shangwe la namna yake pale mama Samia alipotambulishwa Kama Iron lady , uwanja ulisimama kwa sekunde karibia 70.
Kwanini Wakenya wameonesha upendo mkubwa kiasi hiki kwa mama la mama.?
Wanabeba mahindi kama ya kwao vile. Wakenya hawajawahi kuwa marafiki zetu.

Wanampaka mafuta Kwa mgongo wa chupa.
 
Na mwanamke ameumbwa kupendwa na kupewa attention na Rutto inaonekana analijuwa hili vyema.

Mama Jana kalala unono sana Kwa attention ile na kupewa fursa ya kutowa hotuba fupi.
Kama wewe unavyompa attention humu?

Ni rais wako hadi 2030
 
Chawa bana, mnadhani hatukuona hilo tukio? Kila kiongozi alipigiwa makofi kivyake, hakuna rais yoyote aliyepigiwa makofi ya tofauti mpaka ulete hizi propaganda za kijinga.
Tatizo tv zao za Chuplichupli zimewaonesha kapande kamaoja ka Mama Samia tu akiingia na pale alipotoa speech yake! Ukiwaauliza Rais Ruto kasema nini wala hawajui chochote kile!!![emoji3][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Chawa bana, mnadhani hatukuona hilo tukio? Kila kiongozi alipigiwa makofi kivyake, hakuna rais yoyote aliyepigiwa makofi ya tofauti mpaka ulete hizi propaganda za kijinga.

Msamehe bure mleta hoja, kwa sasa ndio aina ya watu waliojaa mtaani Mkuu! Praise and worshipers!
 
Kumbe mama Samia sio wa mchezo mchezo.
Uwanja ulilipuka kwa shangwe la namna yake pale mama Samia alipotambulishwa Kama Iron lady , uwanja ulisimama kwa sekunde karibia 70.
Kwanini Wakenya wameonesha upendo mkubwa kiasi hiki kwa mama la mama.?
Sababu ziko kama 2 hivi,

Mosi Rais Samia anaonekana ndio kioo cha uongozi kwa wanawake hasa hapa Africa inayosumbuliwa na mfumo dume.

Hapa Tzn kwa mda mfupi Rais Samia ame deliver na kuongoza vyema kabisa kwenye sekta zote na kumfunika yule Malaika ila sasa wafusi wa Dhalimu wanatafutiza visababi weee Ili kujaribu kuonyesha kwamba eti ameahindwa wakati namba na uhalisia wanajua kamzidi dhalimu waliyeaminisha wajinga kwamba ni second kwa Nyerere wakati alikuwa jizi kubwa..

Sababu ya pili ni kuwezesha kurejesha mahusiano mazuri na majirani hususani Kenya yanayowezesha biashara baina ya pande mbili tofauti na ilivyokuwa kwa Mwendazake..Kenya na Tzn tunategemeana kwa mambo mengi hasa ya kiuchumi..

Na kudhihirisha hilo Ruto alifanya mazungumzo Ikulu na SSH kabla ya kuapishwa na pia nilimuona Rostam Aziz kwenye jukwaa kuu hivyo ule upuuzi wa Kenyatta na yule Mwarabu wa Mombasa kuzuia gas ya Tzn unaenda kuisha.
 
Wanabeba mahindi kama ya kwao vile. Wakenya hawajawahi kuwa marafiki zetu.

Wanampaka mafuta Kwa mgongo wa chupa.

Hivi tunafaham tunacho kitaka? Hayo mahindi ni hisani au wananunua kwa pesa zao? Kama inakukera Fuga kuku upate kuwalisha.
 
Back
Top Bottom