Inashangaza kuona kwamba UWT ni taasisi ya CCM. Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unapaswa kuwa umoja wa wanawake wote Tanzania bila kujali itikadi ya vyama. Wanawake wa CCM waanzishe umoja wao kama ilivyo BAWACHA kwa CHADEMA, n.k.
CCM kiache kupora taasisi na mali nyingine za umma na kuzifanya kuwa mali au taasisi za chama. Kuna viwanja vya mpira kama CCM Kirumba, majengo kadhaa ya umma, n.k. vimefanywa kuwa mali za CCM! Huu ni uporaji wa mali za umma kwa faida ya vyama vya siasa.
Umoja wa Wazazi na Umoja wa Vijana Tanzania pia hazipaswi kuwa taasisi za CCM.