Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

Kwanini vijana wengine kutoka Mazingira magumu huibuka na kufanikiwa?

dgombusi

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
141
Reaction score
200
Kuna vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu lakini wanashinda changamoto na kufanikiwa maishani.

Unadhani ni nini kinachowasaidia kufanikisha haya licha ya changamoto kubwa wanazopitia? Na sisi sote tunaweza kujifunza nini kutoka kwao?
 
Kuna vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu lakini wanashinda changamoto na kufanikiwa maishani.

Unadhani ni nini kinachowasaidia kufanikisha haya licha ya changamoto kubwa wanazopitia? Na sisi sote tunaweza kujifunza nini kutoka kwao?
Kuamini ndoto zao, na kutokata tamaa licha ya kupitia changamoto zenye kukatisha tamaa. Maskini wengi hujikatia tamaa jambo ambalo huzizika rasmi ndoto zao.
 
Baraka za MUNGU
Mungu ana nafasi kubwa katika mafanikio ya mtu, hasa kwa wale wanaomtegemea ili wafanikiwe.
Bidii na kujituma
Mafanikio ya wengi walio kwenye hali duni yanaletwa na bidii kwa kiasi kikubwa.
Mindset Nzuri
Wanaofanikiwa huwa wameweka malengo ya kufanikiwa na akili yao inawaza kufanikiwa ndio maana wanafanikiwa.
Good Timing
Ili kutoka katika hali ngumu vijana waliofanikiwa walijua kufanya jambo sahihi katika wakati sahihi wa kufanya hilo jambo.
Bahati na ngekewa binafsi
Japo wote tunahustle wakati mwingine wanaofanikiwa ni wale wenye bahati, aisee asikwambie mtu kuna watu wana bahati!
Kipaji na talanta
Vijana waliofanikiwa wapo wenye talent zao katika mambo walioyochagua kuyafanya. Wanatumia sauti zao, miguu yao, akili zao ipasavyo. Mifano ni mingi kina Nasibu Abdul,Samatta,Mwakinyo
 
akili, ujasiri, kujituma.
Wanaondika bahati hata uwe na bahati vipi kama uwe huna akili you will never make it!.

Ingawa ni kweli akili, ujasiri, na kujituma ni muhimu, je, huoni kuwa wakati mwingine bahati pia inaweza kuwa kichocheo cha kufanikisha mipango?

Kuna wale ambao, licha ya juhudi na mipango yao, wanahitaji fursa fulani au mabadiliko ya hali ambayo yanaweza kuonekana kama bahati.

Pia, si kwamba tunapuuza umuhimu wa akili na juhudi, bali tunakubali kuwa wakati mwingine kuna mambo yasiyotegemewa yanayoweza kusaidia kufanikisha malengo.
 
Luck comes with risks.
Njia pekee ya kutumia bahati vizuri ni kufanya maamuzi magumu.
 
📌Wagumu hawana FAKE STANDARDS,pia hawana habari ya KURUDISHA MPIRA KWA KIPA,unakomaa na maisha mwanzo mwisho kwasababu unajua ukimess up kule kijijini kwenu MSOTO wake ni bora ufe👋so hawa wasongombikaji(WAGUMU) huwa wanapambania KOMBE kufa na kupona,nyuma mwiko mbele kwa mbele kitafahamika tu!!!

Wamjini/wakishua wao wanatest maji kwa ugoko akiona namna gani hapa huyo anarudi kwa WAZAZI anazeekea hapo kama yule babu wa TIKTOK.

Hi spirit ya kujua ukizingua kuna pa kuegemea inafanya hawa wakishua wanakuwa less AGGRESSIVE na mapambano ya kimafanikio.Zaidi zaidi wakishua wanategemea wizi na dili hawana muda wa kuumiza kichwa!!!
 
Back
Top Bottom