MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Kaka hata wewe ungekuwa kiongozi lazma ungejipendelea.
Huo ndo ukweli.
OK. Bro. nimekuelewa. Ni kwa matumizi ya Kazi/Shughuli zitokanazo na Wadhifa(dhamana) alionao.Ofisi inapewaje nyumba ya kuishi au gari?
Nimesema "Nchi nyingi ipo hivyo" sijasema "Nchi zote" soma tena comment yangu.Nchi zote haziko hivyo, tuchukulie Ujerumani ambao kwa Pato wanatupita kwa kila kitu, mbunge analipwa 10,012.89 Euro kwa mwezi na Kanzela analipwa 351,552 Euro kwa mwaka ambayo ni sawa na29,296€ kwa mwezi. Hawa wote wanalipa nyumba kwa Pesa Zao, gari wanayotupia wanapewa leasing, maana yake wanakatwa kila mwezi kwenye mishahara yao
Mishahara ya kikoloni hiyo bado ipo kwenye mfumo wa kinyonyaji.Kwa nini wazungu wamishenari walijenga shule pamoja na nyumba za walimu, lakini kwa sasa shule za kata zinajengwa porini bila nyumba za walimu?
Mfanyakazi wa ngazi za chini analipwa mshahara mdogo ambao utagharamia kila kitu, ila mkurugenzi wa halmashauri analipwa mshahara mkubwa na marupurupu mengine!
Kwani ujenzi wa nchi unaanzia ngazi ya chini au juu? Binafsi naona unaanzia ngazi ya chini mfano mtendaji wa kijiji, afisa kilimo wa kijiji, mwl, nesi nk. Sasa kwa nini hawa wanalipwa mshahara mdogo kuliko hao wa juu wanaounganisha taarifa?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mbona naona kama serikali ya kikoloni ilikuwa inamnyonya mfanyakazi lakini inatengeneza mazingira ya mtu kuendelea kuishi ili anyonywe, tofauti na serikali katika zama hizi ambapo mtumishi ananyonywa mpaka anajifia kabisa, na serikali haijali.Mishahara ya kikoloni hiyo bado ipo kwenye mfumo wa kinyonyaji.
Sema milele.kwa fikra kama hizo, CCM wataendelea kutuburuza kwa miaka mingi ijayo
Hao ni maofisa wakuu wa serikali,wanahudumia na kusimamia sera kwa nchi nzima,au mkoa,ni tofauti na mkurugenzi wa Idara.Kwanini mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi ma-RPC nk., nk...
Pamoja na mishahara yao minono bado wanapewa nyumba, magari, walinzi, wanalipiwa umeme, maji, matumizi ya simu nk ili hali watu wengine wafanyakazi wengine wa serikali na taasisi zake wanabeba misalaba yao wenyewe?
Why double standards?
Kama kazi yake kuonyesha njia basi ndio maana muhimu alipiwe vyote hivyo Ili asiwapoteze.Lakini kuongoza ni kuonyesha njia...
Eti nawe pia ni great thinker!Kama kazi yake kuonyesha njia basi ndio maana muhimu alipiwe vyote hivyo Ili asiwapoteze.
Haki yake ni kulipwa mshahara stahiki. Hayo mengine awajibike nayo.Hao ni maofisa wakuu wa serikali,wanahudumia na kusimamia sera kwa nchi nzima,au mkoa,ni tofauti na mkurugenzi wa Idara.
Lakini hata kwenye mashirika ya umma,maofisa waandamizi na wao wanapewa masurufu mazito.
Mkurugenzi hawezi kuhudumiwa kama karani au dereva.
Una elimu na umri gani? Umeshawahi kusikia kitu kiitwacho fiscal capture?Eti nawe pia ni great thinker!