Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Ni sahihi kwa viongozi kuingia kwenye kikao cha Mhe. Rais bila diary wala note book? Au protokali ndio inataka hivyo?
Na kama ni protokali mbona Mhe. Rais alikuwa busy kusikiliza na kuandika? Baadhi ya viongozi wanaonekana kwenye TV wamelala kabisa.
Enzi ya utawala wa Mwalimu na hata utawala wa Magu viongozi walijiandaa wakati wote kupokea maelekezo ; leo Mhe. Rais anatoa maagizo hakuna anayechukua maagizo kwa maandishi. Hii haijakaa vyema; inaleta picha kwamba wanaohudhuria hivi vikao wanajua hakuna maagizo watapewa. Lakini pia inapunguza ufanisi kwa sababu ni vigumu kukumbuka kila kilichosemwa kwani si kila kinowasilishwa kipo kwenye ripoti.