Kwanini Vitabu vya zamani vina maudhui ya kitoto sana?

Nirudi kwenye mada kama kichwa cha habari kinavojieleza, nimesoma baadhi ya vitabu vya Kiswahili vya kizamani kama Alfu Lela Ulela, Hekaya za Bunuasi, Safari ya Bulicheka na Mkewe, Alibaba na Wezi 40, Kusadikika na vingine vingi lakini kiukweli nimeshindwa kuvielewa naona kama maudhui yake si ya mtu mzima!

Nimesoma vingi sana baada ya miaka mingi kuona humu JF watu wakivisifisia sana. Hivi vitabu au vimelenga wazee? Au me ndo akili ndogo?

Havijanivutia kabisa yaan ni vitabu vya kitoto
Tatizo ni kuvisoma ukiwa mtu mzima.
 
utakuwa siyo mlengwa- ama utakuwa juu au chini ya umri lengwa
 
Nina uhakika haujasoma kitabu chochote ww ila unaleta ujuaji tu, hivo vitabu ni vya kitoto mno
We uliyevisoma ukubwani ndiye unaleta ujuaji. Mi nina app inavitabu hivyo vyote, so huo uhakika wako kuwa sijasoma... Watu wanajua kuwa ni vya watoto, wanavipenda sababu ya kuwakumbusha mbali. BTW naomba uinstall app. Kuna vitabu vya aina mbalimbali. Kwa vitabu serious napendekeza usome Kiongozi, Sanaa ya vita na Tajiri wa Babeli. Kusoma ni free.

Screenshot_20220223-215040.png
 
Nimesoma hivyo vitabu. Na kile cha Yahana mjinga.

Kiwavi na sungura hahahaha. Mimi ni jini kuu la bahari 7, naweza kumpiga ndovu kwa kidole kimoja na kumsagasaga kifaru kwa unyayo wangu. Kiwavi akimchimba beat simba
Nakitafuta sana hicho cha Yohana mjinga na utiivu wake. Una access nacho?
 
"Paulo usije kucheza na sisi una mikono michafu........" Hii si ipo ndani ya kitabu cha Bulicheka na Lizabeti?
 
Nirudi kwenye mada kama kichwa cha habari kinavojieleza, nimesoma baadhi ya vitabu vya Kiswahili vya kizamani kama Alfu Lela Ulela, Hekaya za Bunuasi, Safari ya Bulicheka na Mkewe, Alibaba na Wezi 40, Kusadikika na vingine vingi lakini kiukweli nimeshindwa kuvielewa naona kama maudhui yake si ya mtu mzima!

Nimesoma vingi sana baada ya miaka mingi kuona humu JF watu wakivisifisia sana. Hivi vitabu au vimelenga wazee? Au me ndo akili ndogo?

Havijanivutia kabisa yaan ni vitabu vya kitoto
Mwenye soft copy ya hivi vitabu naomba anisaidie navyo wadauuu
 
Mmmmh na kile kinachosema Mtu alikufa na kufufuka siku ya tatu je?
Mikate mitano kula watu elfu Tano!
Mtu kutembea Juu ya maji!
Fimbo kugawanyisha bahari!
NK nk

Kile Cha ukifa kama ulikua mwema unaenda Peponi kupata mabikra 72 wa kugegeda na kuogolea kwenye mito ya pombe na kunywa asali na maziwa
Ni vya watu wazima vile?

Vitabu vingi vya Zamani vumejaa hekaya za kitoto Sana ila still Kuna mpaka Wasomi grade one wanaviamini na kuita Imani what a joke!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji91][emoji91][emoji91]
Roho chafu kazini
 
"Paulo usije kucheza na sisi una mikono michafu........" Hii si ipo ndani ya kitabu cha Bulicheka na Lizabeti?
Aidha hicho cha 'Someni kwa furaha' cha kwanza, au cha pili kile chenye ushairi wa 'Mgeni siku ya kwanza..... mpaka siku ya kumi'
 
We uliyevisoma ukubwani ndiye unaleta ujuaji. Mi nina app inavitabu hivyo vyote, so huo uhakika wako kuwa sijasoma... Watu wanajua kuwa ni vya watoto, wanavipenda sababu ya kuwakumbusha mbali. BTW naomba uinstall app. Kuna vitabu vya aina mbalimbali. Kwa vitabu serious napendekeza usome Kiongozi, Sanaa ya vita na Tajiri wa Babeli. Kusoma ni free.

View attachment 2128929
Hiyo app ninayo mbona
Screenshot_20220224-184117_WhatsApp.jpg
 
Nirudi kwenye mada kama kichwa cha habari kinavojieleza, nimesoma baadhi ya vitabu vya Kiswahili vya kizamani kama Alfu Lela Ulela, Hekaya za Bunuasi, Safari ya Bulicheka na Mkewe, Alibaba na Wezi 40, Kusadikika na vingine vingi lakini kiukweli nimeshindwa kuvielewa naona kama maudhui yake si ya mtu mzima!

Nimesoma vingi sana baada ya miaka mingi kuona humu JF watu wakivisifisia sana. Hivi vitabu au vimelenga wazee? Au me ndo akili ndogo?

Havijanivutia kabisa yaan ni vitabu vya kitoto
Jaribu kuweka yaliyoandikwa kwenye vitabu hivyo kwenye matendo halafu uje useme ni vya kitoto
 
Wanadamu wanakua kiakili zama hadi zama.
Akili yako sasa ni tofauti na ya babu yako.
Wewe una akili zaidi na pia technology imepenyesha maarifa kwa kasi sana
 
Mkuu jaymoul heshima kwako.

Vitabu vya riwaya, tamthiliya na tenzi vina pande kuu tatu ambazo ni literal, metaphoric na allegoric.

Nikupe mfano kutoka Kusadikika(Shaaban Roberts-RIP) ambaye kwa maoni yangu ni mwandishi bora zaidi kuwahi tokea kwenye lugha yetu ya kiswahili.

“Huko alimkuta Jeta, mfalme wa Majuju. Tani milioni za miamba, milioni za chuma, milioni za magogo na milioni za maji zilimiminika kinywani kwake kila sekunde na kila sekunde alikuwa akilia njaa, kiu, njaa”.

Literal:- chakula cha Jeta kilikuwa miamba ya mawe, chuma, magogo, na chuma kwa kiasi tajwa huku akishushia na maji kwa kiasi tajwa pia.

Metaphor:- Jeta ni jitu lafi na lisilotosheka. Kuna viumbe wa namna hii hasa katika sisi wanadamu.

Allegory:- Mwandishi anauona ujio wa Industrial Capitalism ambayo haina ukomo katika utafutaji na ulaji(consumption) wa malighafi.

Visome tena hivyo vitabu mkuu na utaona kuna kitu cha kujifunza bila kujali rika au kwamba vimeandikwa lini.
 
Vitu serious hua havisomwi sana... vya masihara ndiyo vinapendwa...
 
Back
Top Bottom