Kwanini vyombo vya habari vya Magharibi havitangazi maandamano yanayoendelea nchi nyingi za Ulaya?

Kwanini vyombo vya habari vya Magharibi havitangazi maandamano yanayoendelea nchi nyingi za Ulaya?

Nikuulize swali na wewe!

Umejificha kona ipi ya dunia ambako umeshindwa kabisa kufuatilia hivyo vyombo vya habari?

Ama unauliza swali ukiwa na agenda nyingine binafsi nyuma ya swali lako?

Maandamano makubwa yaliyopo Ulaya ni ya nchini Ufaransa na yamesharipotiwa mara kadhaa na vyombo vya habari kadhaa maarufu vya nchi hizohizo za magharibi.
 
Hali si Hali Ulaya nzima kutokana na maandamano ya mara Kwa mara kutokana na Hali ngumu ya maisha na mfumuko mkubwa wa bei za Nishati na vyakula..

Kutokana na hilo , vyombo vya Habari vya Magharibi vinaona aibu kufanya coverage huku vikijitahidi kuficha uhalisia wa Hali mbaya za maisha huko kwao wanakojifanyaga wameendelea..

Kuna Maandamano kwenye Nchi zaidi ya 10 huku waandamanaji wakitaka Serikali zao zing'oke..

Afrika itaendelea kuwa Nchi ya ahadi hadi Wazungu waombe poo.👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221018-123920.png
    Screenshot_20221018-123920.png
    236.9 KB · Views: 2
Wewe umezijuaje hizi habari?
Maandamano yanaendelea nchi kama Italy, France na Germany kupinga hali ngumu ya maisha pamoja na NATO, nastaajabu kuona habari hizi hazipewi headline, kwanini ?
 
Hali si Hali Ulaya nzima kutokana na maandamano ya mara Kwa mara kutokana na Hali ngumu ya maisha na mfumuko mkubwa wa bei za Nishati na vyakula..

Kutokana na hilo , vyombo vya Habari vya Magharibi vinaona aibu kufanya coverage huku vikijitahidi kuficha uhalisia wa Hali mbaya za maisha huko kwao wanakojifanyaga wameendelea..

Kuna Maandamano kwenye Nchi zaidi ya 10 huku waandamanaji wakitaka Serikali zao zing'oke..

Afrika itaendelea kuwa Nchi ya ahadi hadi Wazungu waombe poo.👇
Huyo James Melville anazungumzia media zipi? Hajazitaja!

Wewe umechukua opinion ya mtu mmoja kule Twitter ukaifanya kuwa ndio 'fact' wakati ungejituma angalau kidogo tu kutafuta taarifa kupitia vyanzo vingine, kama vile Google, ungefahamu mengi zaidi.

Hivyo vyombo vya habari unavyosema vinaona aibu kutoa taarifa za maandamano ndio hivi hapa chini?

Suala mojawapo ambalo ni la msingi sana ni kuwa, katika hizo nchi za Ulaya (EU) ambazo maandamano yanaendelea, hilo ni jambo halali kabisa kufanywa na wananchi. Ni haki inayoheshimiwa. Wengine huandamana just for fun!

Hizo ni nchi ambazo viongozi wake huwajibika kwa kujiuzulu ama huwajibishwa kwa kura za wawakilishi wa wananchi ama wananchi wenyewe.

Upande mwingine wa tofauti, kuna nchi ambazo maandamano ni haramu hususani yale yanayofanyika dhidi ya serikali. Hata hivyo, wananchi wa baadhi ya mataifa hayo huandamana licha ya mazuio na vitisho vingi.

Ukiona raia wanaandamana dhidi ya serikali yao licha ya risk kubwa na vitisho vingi vya serikali hiyohiyo, ujue kuwa hali ya maisha yao imefikia pabaya zaidi.
 
Zitangaze wewe, haujazuiwa ila ulijuaje kama yapo ikiwa hayatangazwi?
 
Maandamano yanaendelea nchi kama Italy, France na Germany kupinga hali ngumu ya maisha pamoja na NATO, nastaajabu kuona habari hizi hazipewi headline, kwanini ?

Hutawahi kuwasikia wakiponda nchi zao kama media za Afrika zinavyofanya.
 
mscow waliandamana zaid 2000 wakawekwa ndani.
beijing waliandamana 300+ ndani
irani wameandamana 50+ unarmed died
ulaya watu wanapewa fursa ya kupaza saut zao kueleza hisia zao
sio habari kubwa kuskia maandamano ulaya ndomana hazitangazwi kwa mbwenbwe had ukute bbc wanaweka kambi kabisa eneo la tukio.
mfano
maandamano ya haki kutoa mimba usa
maandamano ya vikwazo vya covid ufaransa
nk. hutaskia violence yoyote.
 
Kuna watu hawajui kuwa katika nchi kama za Umoja wa Ulaya, maandamano ni haki ya msingi sana ya kiraia na haki hiyo inalindwa na kuheshimiwa sana.

Kuna wakati maandamano huwa kama burudani tu, watu wakijumuika na kufahamiana. Vyombo vya dola hutoa ulinzi full-time.

Huwezi kufananisha na zile nchi ambazo maandamano dhidi ya serikali ni haramu, uhaini n.k.
 
Si baba zetu hawa mataifa ya magharibi, watupe mingi misaada huku kuna njaa hatushibi, tukienda kinyume nao watuite magaidi. Majasiri ka Mugabe kuwakandamiza mzidi, majasiri ka Gaddafi kuwakandamizi mzidi. Bado ngware, msijisahau.
 
Wavaa kobazi wanasahau kuwa hawa wazungu wanaoandamana ni wale wanaopinga suala la uhamiaji pia yaani wenye msimamo mkali, hivyo hawajui pia wanataka hao wavaa kobazi wenzao waliopewa hifadhi ulaya wanaoweza kufurushwa na waandamanaji
 
Kuna watu hawajui kuwa katika nchi kama za Umoja wa Ulaya, maandamano ni haki ya msingi sana ya kiraia na haki hiyo inalindwa na kuheshimiwa sana.

Kuna wakati maandamano huwa kama burudani tu, watu wakijumuika na kufahamiana. Vyombo vya dola hutoa ulinzi full-time.

Huwezi kufananisha na zile nchi ambazo maandamano dhidi ya serikali ni haramu, uhaini n.k.

si ajabu kuskia viongozi na wanaharakat katika maandamano hayo wanakamatwa watamunywa kende had waseme nini kimewasibu had waandamane.

nchi za magharibi ni mfano mzur wa democrasia.
 
Back
Top Bottom