Kwanini vyoo vya umma vinatengwa kwa jinsia ya wanaume(ME) na wanawake(KE)?

Kwanini vyoo vya umma vinatengwa kwa jinsia ya wanaume(ME) na wanawake(KE)?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwanini vyoo vya umma vya watu wazima huwa vinatengewa kwa jinsia ya Wanawake(KE) na Wanaume(ME)?

Kuna tatizo gani kwa wanaume na wanawake kutumia choo kimoja?

Kwanini vyoo havitenganishwi vya watoto na watu wazima?
 
Kwa nini vyoo vya umma vya watu wazima huwa vinatengewa kwa jinsia ya Wanawake(KE) na Wanaume(ME)?

Kuna tatizo gani kwa wanaume na wanawake kutumia choo kimoja?

Kwa nini vyoo havitenganishwi vya watoto na watu wazima?
Utajisikiaje unaingia toi unakuta dadako anakata gogo au lets say mkubwa zaidi yako?? Wa jinsia tofauti
 
Una hoja.

Nafikiri chamsingi ni watoto wadogo wawe na maeneo yao maana kuchangia na watu wazima kuna maradhi hasa kwenye hizi public.

Ke na Me ibaki hivyo hivyo, maana tayari ni jinsia mbili tofauti inaweza kuleta hisia na kusababisha ubakaji.
 
Privacy, uhuru na heshima.
Hakuna busara kuangalia mapaja ya wanawake ovyo ovyo.Vyoo vya uma mara nyingi ni matumizi ya wengi..tena akili tofauti - mtu mwingine anajirekebishia kwenye corridor - wengine hata kumsikia tu anajisaidia ni aibu.Ni heshima tu.
1.Hospitalini kuna wodi za wanawake na wanaume
2.Vyuoni: Wakaka na wadada wanalala tofauti
3.Nyumbani: Watoto wa kike na wa kiume hawalali chumba kimoja.Wasukuma watoto wa kiume wanalala nje kabisa.
Ni ustaarabu na utu.
Hata huku majumbani siku hizi kuna master..baba, mama hatuchangamani na wengine...Sababu ni heshima
 
Kuna wakati binadamu akili zinakuwa 0% na pindi hii ndio neno umma linatofautisha vyoo.
Usipotenganisha huduma za faster zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba wengine wanaweza kosa vyoo vya kutumia kwa kuwa watu wataanzisha huduma tofauti na ya choo. Watu watainamishwa na kubaniwa ukutani sana. Sasa fikiria vyoo hivyohivyo viwe vinatumika na watoto pia. Watakuwa wanajifunza nini?
 
Basi na mimi ngoja niulize "kwa nini kusiwepo na vyoo vya wazee na vijana"? Hivi ni busara kweli kwa mimi mzee kutumia choo kimoja na vijana!!
 
Kuna shule nyingi tu nimeziona wamejenga majengo matatu ya choo. Kuna jengo la chaoo cha wasichana tu na ndani kuna vyumba vitano vya kujisaidia kikiwemo chumba cha walemavu tu na chumba cha kubadilisha taulo za kike na kuzihifadhi mule tayari kuchomwa moto kama takataka. Hali kadhalika wanafunzi wa kiume nao wana jengo lao la choo chenye vyumba sawa na wasichana, wana chumba cha walemavu. Walimu nao wana jengo lao lenye vyumba vitatu, chumba cha wanawake, chumba cha wanaume na chumba cha walemavu, ila walemavu wote ke na me wanachangia chumba, tofauti na vyoo vya wanafunzi walemavu wavulana na wasichana hawachaogii choo
 
Sishangai kua na vyoo vya wanaume na vyoo vya wanawake lengo zaidi ni kulinda wanawake juu ya upuuzi wa hiyo gender nyingine isiyoweza kuhimili tamaa zao za kingono,

Lakini binafsi ikitokea nimetumia choo cha umma hua natumia cha wanaume kwa ajili kuna usafi angalau tofauti na kule kwingine
 
Kuna siku niliingia choo cha kike, sehemu fulani nilikutamo pia wameweka ndoo ya tupia pedi, ndo nikajua kumbe umuhimu upo wa kutenganisha,

Kwaajiri ya dada zetu kujistiri

Ni muhimu sana kuwepo na utengafu hasa sehemu za umma
 
Kwa nini vyoo vya umma vya watu wazima huwa vinatengewa kwa jinsia ya Wanawake(KE) na Wanaume(ME)?

Kuna tatizo gani kwa wanaume na wanawake kutumia choo kimoja?

Kwa nini vyoo havitenganishwi vya watoto na watu wazima?
Ustaarabu, kujisitiri n.k ndio sababu kubwa

Kwa wanaume ni kawaida kukuta mtu kashalimwaga wese anakung'uta pipe sasa tungeshea we ingekuwa kuwatesa kisaikolojia wanawake na kuhofia usalama wao

Pata picha unaingia kwenye choo cha kushea usiku unakuta jamaa refu kubwa jeusi limemaliza kuchimba dawa limeshikilia bonge la mgomba analikung'uta

Huo mshtuko itakuwaje, una hakika gani kuwa mwamba atasepa mazima au atakusubiria nje akuweke

Kwa kifupi ni mengi
 
Kwa nini vyoo vya umma vya watu wazima huwa vinatengewa kwa jinsia ya Wanawake(KE) na Wanaume(ME)?

Kuna tatizo gani kwa wanaume na wanawake kutumia choo kimoja?

Kwa nini vyoo havitenganishwi vya watoto na watu wazima?
Duuuh! Ila ndiyo hivyo tumetofautiana akili na uelewa,CCM hoyee
 
Back
Top Bottom