Kuna shule nyingi tu nimeziona wamejenga majengo matatu ya choo. Kuna jengo la chaoo cha wasichana tu na ndani kuna vyumba vitano vya kujisaidia kikiwemo chumba cha walemavu tu na chumba cha kubadilisha taulo za kike na kuzihifadhi mule tayari kuchomwa moto kama takataka. Hali kadhalika wanafunzi wa kiume nao wana jengo lao la choo chenye vyumba sawa na wasichana, wana chumba cha walemavu. Walimu nao wana jengo lao lenye vyumba vitatu, chumba cha wanawake, chumba cha wanaume na chumba cha walemavu, ila walemavu wote ke na me wanachangia chumba, tofauti na vyoo vya wanafunzi walemavu wavulana na wasichana hawachaogii choo