Waafrica ni watu wenye uwezo mkubwa na wamejaliwa mali nyingi na ustahimilifu wa mazingira magumu. Sifa hizo zote kwa karne nyingi zimekuwa ni hofu kubwa dhidi ya wazungu.
Wanajua tukiweza kujitambua na kuendeleza raslmali zetu watakuwa na wakati mgumu sana, na pengine tunaweza kuwaangamiza na wakapotea, wao ni dhaifu, nchi zao hazina raslmali na hata hali za hewa kwao si rafiki.
Ili wao kuishi wanatutegemea kwa aslimia kubwa, hili liliwafanya wao kujihami mapema. Wakahakikisha wanapora mali zote na kutengeneza mazingira ambayo hatutakuwa kitu kimoja.
Mfano ni kutugawa katika nchi nyingi na kuhakikisha hatuongei lugha moja. Wao wameungana na wanaongea lugha moja, lakini Tanzania na Angola au congo mpk Cameron tuna lugha tofauti tofauti. Vile vile siasa zetu hazikubaliani. Jumuiya ya Africa mashariki tu imeshindikana.
Hivyo yote unayoyaona nchi za watu weusi ni ufefhuli wa mtu mweupe.
Alihakikisha kupitia Dini, vita na saikolojia anatutawala tusije amka na kujitambua kwa hali yoyote ile.
Alitutumikisha kama watumwa, jambo hili lilitudumaza watu weusi na kutuchelewesha kwa takribani miaka hata elfu moja nyuma dhidi yao. Ni kama unaanza mashindano ya mbio halfu mtu anakusukuma unaanguka.
Unatibiwa mpka unakuwa sawa then unaambiwa uendelee na mbio, huku mpinzani wako wakati wote huo yeye anakimbia kwa kasi kuelekea mwisho wa pambano, huku wewe ukikimbia kwa kuchechemea japo unauwezo na sifa zote za kushinda.
Naishia hapa, usijidharau. Tunafanyiwa rafu nyingi sana, kuhakikisha hatutoki hapa tulipo, maana wanajua tutakapotoka wao hawatakuwepo tena.