Sorry kwa watakao feel offended
Africa kuna nchi 54. Nje ya Africa nchi ambazo zina jamii ya watu weusi
Ni za visiwa vya Careebian kama Jamaika , Haiti Buhamas.
Lakini zooteee hizo hamna hata nchi ambayo ni developed nation hata moja!!
Matatizo ya Tanzania , Zimbabwe Congo Namibia sijui Africa ya kati ni yale yale na ya Haiti ni yale yale.
Itoe South Africa ambayo waanchi wake weusi hawamiliki asilimia 80 ya uchumi!! Ukiwa umehodhiwa na wazungu.
Jibu kama mtu usie na mihemuko!!
kwa wale waliowahi kuishi America. ulitakiwa unapojumuisha watu weusi ujumuishe na African Americans. wale jamaa wapo ambao mzungu hata akiwa genius hatii mguu, kina Obama, Kina Condoresa Rise, na wengine wengi, isipokuwa ni wale tu wanaotoka familia yanye kipato, na wengi wao utakuta ni mchanganyiko wa mzungu na mweusi. nimesoma na African Americans, wapo vizuri sana kichwani kwa wale wanaoenda shule na wapambanaji balaa.
kwa utafiti ambao tayari ulishafanywa, ili mtu awe na uwezo wa akili kiwango cha juu pamoja ambavyo pia vinaendana na ustaarabu, ipo determined na aina ya maisha aliyokulia tangu akiwa tumboni mwa mama yake.
kwa kifupi, aina ya vyakula tunavyokula ndivyo vinavyodetermine development ya ubongo. mtoto tangu akiwa tumboni anatakiwa kula vyakula vitakavyoboresha ubongo wake, na vyakula hivyo vingi ni vile vyenye omega3 inayopatikana kwenye ndizi, mafuta ya samaki na parachichi na kiini cha yai. sio hivyo tu, wakati anakua, anatakiwa kula chakula bora, omega3 isipungue pamoja na proteins za kutosha kwasababu ndizo zinamfanya akue.
wakati anaendelea kukua, usimbanie, kila anachotaka kufanya unamchapa, akitaka kucheza michezo fulani unamkataza, etc, kwa watoto wa kibongo, wengi wanalelewa na housegirls na mzazi atamwangalia mtoto akirudi, ukimpatia chakula housegirl anakula chote anampa mauji anashiba, uji usio wa lishe hauna faida na haumfanyi akue wala kudevelop ubongo wake. ubongo ukilishwa vyema kwa vyakula bora ukakua vizuri mtoto IQ inakuwa juu sana.
kwa Africa, wengi tunakula ili tuishi, nilijifunza kitu kimoja, ukiishi na wachina, utajua kuwa wee unakula tu ili uishi lakini hauulishi mwili wako. jamaa wanaweza kula nyama na samaki ambayo wangekula watu wawili, piga maziwa, piga matunda, tandika tandika balaa, na hata akila kidogokidogo anakula mara nyingi. breakfast yao ya ajabu. na vyote hivyo VINATOKANA NA KIPATO, ukiwa na kipato kidogo hautakula vyakula bora na ubongo wako utadorora. wazungu wengi wana uwezo kununua chakula bora kwa watoto everyday na wanawapa nafasi ya kujaribu kufanya mambo mbalimbali, hawachapi watoto na kuwatia hofu kama sisi huku, huku kwetu mtoto anaishi kwa hofu ya kuchapwa tu muda wote na hofu hiyo anakuwa nayo hadi ukubwani. nyumbani, mtaani, shuleni etc anakuwa na hofu tu na kufokewa na kuchapwa hivyo na ubongo wake pia unakuwa hivyohivyo,
vijijini kwetu tulikozaliwa huko unaamka asubuhi unakula viazi au ugali unaenda shamba. kitu pekee utakachofaidika ni mboga za majani ila ugali/viazi ni wanga haujengi mwili, kwahiyo ubongo haulishwi ndio maana vichwa vigumu kuelewa.
tafiti zilifanywa kwenye mikoa ambayo watu wanaishi milimani, uwezo wa kufikiri ni mdogo kwasababu ya weathering ya udogo kwenye mazao wanayolima, madini ya chuma yanachukuliwa na mvua na kupelekwa kwenye mto hadi mabondeni huko, wenyewe kile wanachokilima kule juu hakkina madini ya chuma ambayo pia yanasaidia development ya ubongo. labda kwa siku hizi chumvi wamelazimisha lazima iwekwe madini ya chuma sio kama sisi zamani tulikuwa tunakula ile ya mawe.(wahenga tu wataelewa hapa).
kiujumla, watu weusi kwenye nchu ulizotaja za carrebeans na africa, utaona uchumi wao upo chini sana, hawana kipato cha kuwafanya wale balanced diet, na balanced diet ndio inafanya watu wawe na afya ya akili na ustaarabu.
chukua mfano wa Nigeria, kule kuna vyakula vingi (ni kama tukuyu na bukoba), walipima watu duniani iq, mwaka juzi kuna mtoto mmoja toka nijeria aliibuka kinara. wanachofanya wenzetu wanaiba sana nchi za watu wanatajirika na kurudi kwao. nchini kwao pia kuna matajiri wa kufa mtu kwasababu wanafanya sana kazi, hivyo ukiamua kuchukua sampuli za vipimo, chukua waafrica toka familia mambo safi, waamerica weusi na wanijeria utapata jibu.
on the other side, kuan mambumbumbu ulaya mashariki huo kwenye umasikinini huko, ile former USSR kuna baadhi ya nchi ni maskini kidogo, huko aisee kuna mambumbumbu bora hata waafrica. same applies to Arab countries wale masikini wanajua tu kuswali akili zingine hawana kabisa. tulishe watoto vyakula bora ili wasihangaike baadaye.