Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k?

mngekuwa serious mngeanzia kwenye mavitu yao waliyowaletea kwanza,leo hii kujifanya unakataa majina wakati una gari lao,nguo zao,viatu zao,mpaka perfume umepulizia za kwao ni kuivuruga akili yako na kuipa kazi nyingi zisizo na maana.
Utetezi huu wa kindezi sana, sisi tulikuwa mbele kiteknolojia kabla hawajatuvuruga

Hata wasingekuja tungefika maendeleo haya sisi wenyewe
 
Mimi niona jina zuri kwa lugha yoyote si kosa kinachomata na maana Tu

Mfano
Happy kingereza

Saeida kiarabu

Furaha Kiswahili

Uwe muislam ao mkiristo sababu ata kwa kimakonde,kizigua n.k halina tofauti kimaaana zaidi ya matamshi na lugha
Ulishasikia mzungu anajiita furaha? Ila nyie kutwa kujiita Happy what for?!
 
Majina asilimia kubwa ni maneno ya lugha ya mahali; yana maana fulani nzuri au mbaya tokana na yule anayetoa. Mfano jina Messi umaarufu wake ndio uliolikuza jina, kiasi cha kwamba watu wameanza kuwaita mtoto Messi.
Mitume au manabii unaowasema walikuwa majina hayo hata kabla hawajawa nabii au mtume. Mfano Muhammad ni jina la Kiquresh (lugha ya Kiarabu) aliitwa hivyo hata kabala hajawa mtume; au Yesu (jina la Kiyahudi -"Jehoshua") yenye maana nzuri. Majina yalikuwepo hata kabla yao. Maana yangu ubora wa mtu hautokani na jina lake. Watoto wanaoitwa Muhamad tungewakuta wote ni manabii lakini sivyo.
Kutunza lugha zetu pia ni kwa njia za majina.
Wengi wanaobeza maneno mazuri ya lugha zetu ambayo tungetumia kuwapa watoto hata atakapokuwa maarufu watu watayafuata. Usibeze lugha yako. Dini ni nzuri na mimi muumini mzuri wa dini ila naheshimu lugha yangu na kuitumia hata kumwomba huyo Mungu wangu.
Ommy Dimpoz anagopa kuitwa OMARI MASHAMUSHAMU NGUZII

NASIBU AETI diamond

abduli -Dully

mi naona wangebali dini tu waende huko kwa wenye hayo majina.
 
Jina ni neno au maneno anayopewa mtu au kitu au hali Fulani

Nataka kujikita kwenye jina tunalopeana watu.

Kwanini Waafrika tunapenda sana kuwapa watoto wetu majina ya Ulaya, Asia n.k., lakini sisi tuna maneno katika lugha za Kiafrika.

Kwanini usumbuke uingie kwenye mtandao na penginepo.

Tanzania tuna lugha nyingi maana tuna maneno ambayo tungetumia kuwapa watoto wetu.

Hatuwi wa maana ati kwa kuitwa Zebedayo au Hasani au Rebecca au Salha nk

Hatuwi wacha Mungu wazuri kwa majina hayo.

Mtu akiishi au akafuata ya huko nje tunamkandia, vipi kuhusu jina mwanao.

Natamami tubadilike, kama wewe ni Mgogo au Mfipa au Mmakua nk tumia neno ambalo unalijua maana take na unalifurahia.

Tuache ushamba wa kupenda tusivyovijua
Mkuu alikuwepo Msomi mmoja anayefahamika kwa jina la IBN KHALDUN yeye alieleza kuwa;

Moja ya dalili ya jamii/Ustaarabu uliofeli kuendelea ni kuacha mila zao na kuiga zile za jamii au za ustaarabu unaosemwa kuwa umeendelea.
 
Back
Top Bottom