Kwanini waajiriwa wengi wakistaafu lazima wapitie msoto mkali wa kiuchumi?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Habarini,
Mfano, Utakuta mtu amemaliza chuo kapata kazi yenye mshahara mzuri, kila mwaka anapanda vyeo kazini, anakuwa na akiba ya pesa nyingi benki, huku mshahara ukiendelea kuingia, ghafla mkataba wa kazi ukiisha au akistaafu hata kama ana akiba hata kama ni ya tsh millioni 400, na magari ya kutembelea, anaanza kuuza magari, hadi yanaisha, kila akifungua biashara, biashara zinafeli, kama mstaafu ni mzee, kisukari na presha, vinakuja na kifo cha fasta.. wengine wanaishia kuomba omba kwa ndugu na kutegemea watoto wao ili ku-survive.

Yaani wakistaafu ni kama mikosi inakuwa inawaandama..

Wakistaafu wanakua kama wanachuo waliomaliza chuo wakakosa ajira.

Wastaafu wachache sana wanaweza kubalance mambo yao ya kifedha yasiyumbe sana hata wakistaafu.

Shida inakuwaga wapi?
 
Tatizo ni pale unapokuwa huna plan kabisa na kuona miaka 70 ni mbali sana

Akiba ni muhimu sana na kufungua biashara baada ya kustaafu labda umpe mmoja wa watoto wako unaemuamini
Kufungua biashara usiyoijua na sura ya uzee hutoboi bora ukae shamba tu uliloliandaa miaka ya nyuma
 
Maziwa ya mshahara mkuu,Sasa umekata!
 
Maisha ya kustaafu hayazoeleki.

Hii pia inafanya wastaafu wengi kuomba mikataba.

Kipekee Mamndenyi anamshukuru Mungu sana, hata kuweza kuhimili misukosuko ya baada ya kustaafu.

Mamndenyi amekuwa mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za Mungu.

Naomba mialiko.🙏🙏🙏
 
Hakuna tajiri aliyeajiriwa, refer forbes
Kuhimili sakata la maisha lazima ujue namna ya kujitafutia mwenyewe, kuajiriwa ni sawa na kifaranga cha kuku kinavyolelewa na mama yake, siku mama yake akifa, kifaranga kinapata tabu.

Mfano mmoja mdogo:-

Kuna rafiki yangu aliajiriwa na kampuni x, na hiyo kampuni ilimfanya aishi mbali na familia yake; alichofanya alianza kujitathmini kuwa anaweza kufanya nini katika kujiajiri; akagundua anaweza kuendesha hiace kama daladala, alichofanya alipambana mpaka akapata fedha ya kununua hiace, na aliponunua hiace aliacha kazi na akaenda kujumuika na familia yake; kwa sasa yeye ndio amejiajiri kwenye hiyo hiace na anaishi kwa furaha huku akiendelea kusomesha watoto wake sekondari.
Kwake hana stress ya ajira wala ya kuachishwa kazi.

Muhimu kwa sasa kwa vijana, ni kufanya maamuzi magumu; kujiajiri kunaleta heshima.​
 
Ukijiandaa kwamba kuna siku utastaafu na kujua Nini Cha kufanya, wengine wakiambiwa wanakaribia kustaafu huukana umri hata kwenda mahakamani kuapa kwamba alikosea!Ili mradi aongezewe muda!too late!
 
Unatakiwa ukistaafu, ukawe mkurugenzi kwenye kampuni yako iliyo hai, kama ulikuwa unalipwa milioni 7+, tunategemea uwe na kampuni inayozalisha na kupeleka bidhaa nje.
 
Hili jambo acheni tu, jirani yangu ni profesa mstaafu wa mzumbe dsm baada ya kustaafu miaka 5 iliyopita nimemuona dhahiri hayupo sawa,kakonda ghafla kazeeka zaidi analalamika maisha magumu, yote tisa 10 babu yangu ni balozi mstaafu ni mwaka wa 10 sasa toka astaafu zile pesa za kila mwezi za wastaafu zikichelewa analalamika ile mbaya sasa kachoka ana nyumba upanga lakini kodi yake anaona haitoshelezi mahitaji ya familia, ukimpa 200k anakupigia simu kukushukuru.

Nb. Maisha ya ajira muokozi pekee ukistaafu ni nyumba za kupanga kwasababu unapokuwa kwenye ajira kupata nafasi ya kufanya na kusimamia biashara ni ngumu sana.
 
Habarini,
Mfano, Utakuta mtu amemaliza chuo kapata kazi yenye mshahara mzuri, kila mwaka anapanda vyeo kazini, anakuwa na akiba ya pesa nyingi benki, huku mshahara ukiendelea kuingia, ghafla mkataba wa kazi ukiisha au akistaafu hata kama ana akiba hata kama ni ya tsh millioni 400, na magari ya kutembelea, anaanza kuuza magari, hadi yanaisha, kila akifungua biashara, biashara zinafeli, kama mstaafu ni mzee, kisukari na presha, vinakuja na kifo cha fasta.. wengine wanaishia kuomba omba kwa ndugu na kutegemea watoto wao ili ku-survive.

Yaani wakistaafu ni kama mikosi inakuwa inawaandama..

Wakistaafu wanakua kama wanachuo waliomaliza chuo wakakosa ajira.

Wastaafu wachache sana wanaweza kubalance mambo yao ya kifedha yasiyumbe sana hata wakistaafu.

Shida inakuwaga wapi?
Ajira ni utumwa inakunyima street hustles na maujanja.. Unakuwa conditioned na timetable ya kazini bar nyumbani nine hours 5/7 a week..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio wote bro, wanaopitia dhahama hizo ni wazee wa mwaka 47! Wa sasa hv watu wameishajanjaruka, wanaelewa, kiinua mgongo sio pesa ya kujengea nyumba, kununua gari au kuanzia biashara!
Kama unaendeleza sawa!
 
Ndio maana serikali ikaona ilete kikokotoo. Upate 30% ya marundo yako ukistaafu, huku ukiendelea kupata robo tatu ya mshahara wako hadi unakufa. Ila wajinga wachache wanataka wapewe hela yote ili wamalize ndani ya mwaka then wakose hata miatano ya chumvi.
 
Tatizo ni pale unapokuwa huna plan kabisa na kuona miaka 70 ni mbali sana

Akiba ni muhimu sana na kufungua biashara baada ya kustaafu labda umpe mmoja wa watoto wako unaemuamini
Kufungua biashara usiyoijua na sura ya uzee hutoboi bora ukae shamba tu uliloliandaa miaka ya nyuma
Eti 'na sura ya kizee, hutoboi' .mbona sisi wastaafu tutakoma kuringaaa
 
Naona Majibu mengi hapa yamekuwa yakufikirika zaidi, they are not realistic

Nadhani kuna haja ya kupata wastaafu wenyewe kuwauliza ili tupate majibu sahihi. Sio vibaya kukiri kuwa kuna mahari ulikosea ili kusaidia wengine wasikosee.

Ndiyo maana akina Ben Mkapa and like wamewahi kuandika vitabu kuwahusu.
 
Back
Top Bottom