Kwanini wabongo hawaweki wazi bei ya bidhaa zao mitandaoni?

Nimeona huku Twitter watu wanalalamika. Hili pia nimeliona sana mtandaoni. Shida nini?
Mosi, Elimu ndogo ya biashara ni tatizo kwa hili taifa, watu wengi biashara kwao ni kama Plan B.

Pili, kuna wauzaji ambao hajaweka bei na hata ukiuliza bei pia bado hakujibu chochote.

Tatu, Watu wengi wanafanya biashara kimazoea, so wao wanaona kawaida tu.

Nne, Kuna wafanya biashara anakutajia bei kutokana na ulivyokuja (MAWINGA), so akiweka online bei hatapata faida, maana kuna malofa wake anowapiga bei kubwa atawakosa.

Tano, Wateja pia ni wasumbufu, muuzaji anaweza andika bei, ila bado mteja akauliza tena bei.

Sita, Wauzaji wanatafuta engagement na wateja, kitendo cha wewe kuuliza bei, kinaweza jenga uhusiano mzuri baina yenu endapo atakujibu ontime, kuliko ukaona bei halafu ukapita.

Mwisho, Wauzaji wanatenganisha wateja miyeyusho na wateja serious.

Infact Kwao wauzaji: BAYA LISILOWADHURU, NI JEMA LISILO NA FAIDA.
 
Hapo mwisho natofautiana nawe. Mara nyingi ukitaja bei wateja watakaokuja ni wale serious. Usipotaja na umelipia tangazo, basi utapata wateja ambao ungeisha wachujq, hela yako itaenda bure kwa sehemu kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…