Ndalilo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,343
- 7,516
Raisi wa upande gani anaweza kutoka upande wowote? SMZ haiwezekani atokee Tanganyika, wa JMT, anatokea kokote, nadhani ndo imeishia hapo sio?😄Rais anaweza kutoka upande wowote wa Muungano. Tunachotaka kujua ni kwa nini wazanzibari wajadili mambo ya Tanganyika yasiyowahusu?
Sasa, kama umetambua hizo mbili tu, jua kuwa hakuna Bunge la Tanganyika na hivyo hakuna raisi wa Tanganyika!
Kinyume chake, bunge la JMT liwe na session 3, kwaajili ya Muungano, kisha Tanganyika affairs and then Zanzibar affair....ambapo hai-make sense sio?
- Kwamba Wawakilishi kule SMZ wana bunge lao, bunge la Wawakilishi Tanganyika(existence ya waTanganyika ni valid na legit kama mnaitambua Zanzibar na si Tanzania Visiwani) hamna.
Raisi wa JMT ni mzanzibari, raisi wa SMZ ni mzanzibari, wenyewe wanasema mawaziri 8 wa JMT ni wazanzibari.....
- Raisi wa JMT anazindua shule zisizo kwenye muungano upande wa pili!
Bunge la JMT lina tofauti gani na Baraza la Mawaziri kiutendaji?
- Sijawahi sikia Baraza la mawaziri wa Bara wamekaa na raisi anayeshughulikia Bara kujadili mambo ya Bara!
Labda iwe hivi; Raisi wa JMT avae kofia mbili, ya JMT na Tanganyika(Hakuna ruhusa Mkaazi kuwa raisi wa JMT)
- Awe na Makamu wa JMT ambaye ni raisi wa SMZ(Strictly Mkaazi)
- Tuwe na PM wa Bara, PM Visiwani(Nadhani ndo muelekeo kwa sasa, Naibu waziri mkuu ni chambo ili mzoee) Zenji walikuwa na Waziri kiongozi.
- Huku Bara, toa wakuu wa mikoa wote na structure nzima ya mkoa, anzisha wakuu wa Kanda. DC aripoti kwa mkuu wa Kanda kiutendaji, kuwe na chief of staff mmoja wa kanda, kisha HRs wa wilaya etc
Mambo ya Muungano yapungue, pande zote zichangie gharama za kuendesha serikali ya JMT, kila mtu asimamie mapato yake.
Ajira za Muungano zisiwe 71% kwa 29%(nadhani iko hivi kwa sasa) Wazanzibar wanapaswa kupewa 2% ya ajira zote zinazohusu Muungano tu!
La, sahau yooote; wapeni nguvu Madiwani, wawe na Bunge kubwa lenye nguvu, maamuzi ya Raisi wa JMT-Bara yawe questioned na Bunge la madiwani! Madiwani wateue wabunge wa Bara kwenda Bunge la JMT.
Kadiri unavyojaribu kurekebisha, unaacha maswali mengi!