Kwanini wabunge wa Zanzibar wasitoke nje ya Bunge yanapojadiliwa mambo ya Tanganyika?

Kwanini wabunge wa Zanzibar wasitoke nje ya Bunge yanapojadiliwa mambo ya Tanganyika?

Mbunge wa manyoni magharibi yupo kwa maslahi ya wana manyoni magharibi tu. Ikiwa hoja ipo sawa, hao wa raha leo wanakuwa hawana madhara kwenye mambo yasiyohusu muungano, ila hawawezi kutolewa nje kwa kuwa hawawezi kujua ni muda gani au ni kwa mchango upi maslahi ya majimbo yao au ya nchi yao yanaweza kuguswa, hivyo watabaki kikaoni muda wote kulinda maslahi yao.
Si ipangwe ratiba tu. Muda wa kujadili mambo ya Muungano ujulikane na uwekwe muda wa kujadili mambo ya Tanganyika.
 
Ni upumbavu walio nao mboga mboga kuendelea kuwa ng'ang'ania wanywa urojo na wakati hawana faida yoyote ile kwa nchi zaidi ya hasara
 
Mkuu hiyo ni hoja!
Nadhani kulitakiwa kuwe na mabunge matatu!
Bunge la Bara,Baraza la Wawakilishi na Bunge la JMT.
Lakini kwa akili hizi za kijani sijui.
 
Yanapojadiliwa mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano, ni kwanini wabunge toka Zanzibar wasiwe wanatoka nje ya bunge na kuwaachia wabunge wa Tanganyika kujadili mambo yanayowahusu watanganyika?

Ni sawa wabunge toka nchi nyingine kujadili mambo yasiyowahusu ya nchi nyingine?
Soma Katiba ya JMT, wala usihangaike. La kufanya: Piga kampeni ya mabadilko ya katiba au ya kuvnja muungano.
 
Kama Watanganyika hatujalongwa,basi tuna matatizo ya akili.
Wao wanasikiliza na kujadilinmambo ambayo siyo ya muungano,tunawaangalia na kupiga makofi😳
 
Kama Watanganyika hatujalongwa,basi tuna matatizo ya akili.
Wao wanasikiliza na kujadilinmambo ambayo siyo ya muungano,tunawaangalia na kupiga makofi😳
Tatizo ni CCM. CCM ni chama Cha wazanzibari watu wa Tanganyika hawana sauti kabisa.
 
Kama sitakuwa mimi, basi tegemea siku moja kutokea Rais nwenye maono kama haya ya kwangu. Unyonyaji kwenye karne hii ya 21 haukubaliki. Kila nchi ile kwa jasho lake.
Tunamsubiri kwa hamu ili avunje huu muungano.
 
Back
Top Bottom