Kwanini wabunge wa Zanzibar wasitoke nje ya Bunge yanapojadiliwa mambo ya Tanganyika?

Si ipangwe ratiba tu. Muda wa kujadili mambo ya Muungano ujulikane na uwekwe muda wa kujadili mambo ya Tanganyika.
 
Ni upumbavu walio nao mboga mboga kuendelea kuwa ng'ang'ania wanywa urojo na wakati hawana faida yoyote ile kwa nchi zaidi ya hasara
 
Mkuu hiyo ni hoja!
Nadhani kulitakiwa kuwe na mabunge matatu!
Bunge la Bara,Baraza la Wawakilishi na Bunge la JMT.
Lakini kwa akili hizi za kijani sijui.
 
Soma Katiba ya JMT, wala usihangaike. La kufanya: Piga kampeni ya mabadilko ya katiba au ya kuvnja muungano.
 
Kama Watanganyika hatujalongwa,basi tuna matatizo ya akili.
Wao wanasikiliza na kujadilinmambo ambayo siyo ya muungano,tunawaangalia na kupiga makofi😳
 
Kama Watanganyika hatujalongwa,basi tuna matatizo ya akili.
Wao wanasikiliza na kujadilinmambo ambayo siyo ya muungano,tunawaangalia na kupiga makofi😳
Tatizo ni CCM. CCM ni chama Cha wazanzibari watu wa Tanganyika hawana sauti kabisa.
 
Kama sitakuwa mimi, basi tegemea siku moja kutokea Rais nwenye maono kama haya ya kwangu. Unyonyaji kwenye karne hii ya 21 haukubaliki. Kila nchi ile kwa jasho lake.
Tunamsubiri kwa hamu ili avunje huu muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…