Uncle Elroy
JF-Expert Member
- May 22, 2016
- 1,177
- 1,090
Leo ningependa nizungumze na ndugu zangu Wachaga na wanipe ufafanuzi kuhusiana na madai yangu.
Ukiwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakutana na machapisho mengi yanayozungumzia sana ndugu zetu Wachaga kwa namna chanya kwamba wana uwezo mkubwa wa fedha nakadhalika na mbaya zaidi wapo ambao wanafikia hatu ya kudharau watu wengine kwasababu ya kasumba hii.
Jambo moja linalonipelekea kuandika article hii ni kwasababu kila napopita mji wa Moshi miaka nenda rudi tangu nikiwa mtoto na sasa ni mtu mzima uko vilevile kwanzia majengo huwa sioni yakijengwa mapya, maghorofa mapya matokeo yake umekuwa ni mji usiokua wala kubadilika kana kwamba hawa Wachaga wameutelekeza.
Wachaga nijibuni kwanini mnasifika sana kwa maendeleo lakini mji wa Moshi ambao ndio utambulisho wenu miaka nenda rudi uko vile vile sasa tunashindwa kuelewa kwanini hamfanani na haya mnayoyasema?
Ningekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro lazima ningewahoji mpaka mnieleze kwanini mji wa Moshi mmeutelekeza huku mkijigamba mna maendeleo makubwa.
Swala la kumiliki rasilimali mikoa mingine ikiweno Dar es Salaam kwa namna ya ndani kabisa ni kwamba mnakweza jiji la Dar es Salaam au majiji hayo lakini asili yenu ambayo ni mji wa Moshi inakufa na mpo kwenye hatari kubwa sana ya kupoteza mji wenu kimaendeleo.
Je hili mnalitambua?
View attachment 2874249
Wafahamu watu 20 Matajiri zaidi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam
Mfanyabiashara wa Kitanzania, Aunali Rajabali. The richest Tanzanian investors on the Dar es Salaam bourse have amassed a total wealth of $81.77 million, according to data gathered at the end of trading on Aug. 20. This is far lower than the wealth local individual investors in other African...
Kwenye hiyo list wachaga wapo 8, wengine sio watanzania. Soma alafu urudi kuedit ulichoandika.