Kwanini wachagga (kabila la mpakani) hawapo Tanzania na Kenya??

Mkuu kwa vile mada inahusu makabila, basi tukubaliane na mimi kwamba mleta mada kakosea. Burundi hakuna kabila linaloitwa waha. Na kama lugha ndio inayoweza kufanya mtu uone kwamba inaweza kuwa na uhusiano na kabila fulan basi hapo pia mleta mada atakuwa amekosea.

Nakupa mfano wa lugha ya yoruba inaongelewa na nchi zaidi ya 3 huko West Africa.Nigeria, Benin na Togo. Lakini bado kuna utofauti wa ki nchi na ki culture baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo.

So kusema eti Burundi kuna waha kwa vile wanaongea lugha inayofanana na kiha hii sio kweli. Waha ni waha, wahutu ni wahutu, watutsi ni watutsi nk.
 
Historia ya Wanyarwanda na Warundi inafanana kwa kiwango kikubwa. Na hayo makabila yalikuwepo kabla hata ya ujio wa wakoloni. Sema wakoloni walichofanya ni kuwagawa katika muonekano wao kwa kusema kwamba huyu mwenye pua nyembamba (mtutsi) ni bora kuliko huyu mwenye pua pana (mhutu)

Kiasili watwa (wawindaji)ndio waliokuwa wakiishi Rwanda na Burundi miaka na miaka. I mean ndio wahadzabe wa huko, hata style yao ya maisha inafanana.

Kisha baadae wakaja wahutu 'wakulima' (bantu) kutoka pembezoni mwa Congo na Centre Africa, kisha watutsi 'wafugaji' (Nilotic) ambao inasemekana walitoka between Somalia, Ethiopia na South Sudan.

Kuhusu lugha ni kwamba hayo makabila mengine yalipofika Rwanda na Burundi yaliamua kufuata lugha iliyokuwa inaongelewa na wenyeji wa wakati huo ambao ni watwa ili kuwasiliana na wenyeji kiurahisi.

Hawa watutsi wanauhusiano fulani na wamasai, japo mazingira ya kijiografia yamesababisha kuwe na muingiliano kati ya wamasai na makabila mengine hivyo kupoteza muonekano walionao watutsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…