Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,870
- 2,122
Leo tuweke mafaili ya ofisini pembeni na tuzungumze ukweli ambao Human Resources (HR) wako hatakuambia kamwe.
Tangu tukiwa shule ya msingi tulikaririshwa fomula moja ya kijinga sana: "Soma sana, piga kazi kwa bidii, bosi atakuona, utapanda cheo na kutoboa kimaisha tuu."
Ila Kwenye ulimwengu wa uhalisia na hesabu za kistratijia, huu ni utapeli wa kiwango cha lami. Mifumo ya ofisi (Corporate structures) haijatengenezwa kumzawadia anayefanya kazi ngumu; imetengenezwa kumzawadia anayejua Kujiuza wale wambea mbea, na wapenda sifa (Visibility) na Siasa za Ofisini (Corporate Politics).
Hebu tuchambue huu ugonjwa wa "Mfanyakazi Bora" kwa jicho la kihesabu na kisaikolojia:
Laana ya Kujua Kazi (The Curse of Competence): Msomi ukijua sana kazi, unajichimbia kaburi lako mwenyewe.
Ukianza kufanya kazi za watu watatu kwa ufanisi wa 100%, bosi wako kamwe hatakupandisha cheo. Kwanini akupandishe cheo (promote) wakati akikuondoa hapo itabidi aajiri watu watatu wapya kuziba pengo lako?
Unageuzwa kuwa 'Punda wa Ofisi' au Msukule (Indispensable Workhorse). Utaletewa maafaili yote magumu utatue, wakati yule jamaa asiyejua kazi anapelekwa semina Arusha na Dubai kwa sababu "ofisi inaweza kujiendesha hata asipokuwepo😒."
Kanuni ya 80/20 ya 'Kuonekana' (Visibility vs Productivity): Wewe 'Great Thinker' unakaa kwenye pc masaa 12 kuandika ripoti nzito ya kurasa 50 inayookoa mamilioni ya kampuni, kisha unaituma kwa email kimya kimya.
Kule juu, kuna "Mjanja wa mjini"/Sungura anasoma Executive Summary ya hiyo ripoti yako, anaandaa PowerPoint ya slide tatu, anaingia kwenye kikao cha Bodi, na kuiwasilisha kwa mbwembwe za Kiingereza. Anapigiwa makofi na kusifiwa Hadi hapo unadhani ni Nani anapewa pongezi na Bonasi mwisho wa mwaka? Wewe uliekesha au yeye? ni yule aliyeuza wazo lako atakuzidi utake usitake. Kwenye siasa za ofisi, "Marketing" ya kazi yako ni muhimu mara kumi zaidi ya kazi yenyewe.
Utii wa Kijinga (Blind Corporate Loyalty): Wasomi wengi wana mapenzi ya dhati na kampuni zinazowalipa mshahara ambao hauvuki tarehe 15. Unakuta mtu anajivunia "Mimi nina miaka 10 kwenye hii kampuni", lakini akiugua leo na kushindwa kufanya kazi miezi mitatu, HR anatangaza nafasi yake kwenye gazeti akiwa bado yupo ICU. Kistratijia, kuwa loyal na kampuni ni sawa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na calculator.
Kampuni inatumia hisabati (faida na hasara), wewe unatumia hisia. Hapo lazima uliwe.
Hasara ya Kutokuwa na 'Scalability' (Kukosa Mizizi): "Hard work" ofisini haina Scalability. Hata ufanye kazi vipi, huwezi kufanya kazi masaa 25 kwa siku. Mshahara wako umewekewa ukomo (Capped).
Wale 'wajinga' ambao hawaumizi kichwa ofisini, wanatumia muda wa kazi kufanya michongo yao ya pembeni kimyakimya, wanapiga simu za madalali, na kujenga biashara (Systems) zinazojiendesha.
Mwisho wa siku, wewe unapata cheti cha mfanyakazi bora na kikombe cha chai chenye logo ya kampuni, wao wanapata hati za viwanja.
Acha kutumia asilimia 100 ya nguvu zako kujenga ufalme wa mtu mwingine huku kwako kukiwa na nyasi. Tumia ofisi kama sehemu ya kupata mtaji, kujenga mtandao (Network), na kujifunza mifumo (Systems) ili uje ujenge himaya yako na kumpa mwanao pa kuanzia. "Hard work" inalipa tu kama unaifanyia kazi biashara yako. Kwenye ajira, "Smart Politics", "Leverage", na kujua kujipendekeza kistratijia ndiyo zinazotoboa.
Wakuu, wangapi hapa wamewahi kufanyiwa umafia wa kuibiwa 'Credit' ya kazi zao na mabosi wao huku wakiishia kupewa "Thank You" kavu? Uwanja ni wenu, tiririkeni.