Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Wafanyabiashara wengi wanaingiza mizigo kwa njia ya magendo, wanazitunza stoo. Wanaweza kupitishia bandarini, njia zisizo rasmi za mipakani, au kwa majahazi. Hawalipi Kodi.

Sasa serikali imeamua kusajili stoo wanazotunzia ili waweze kujua zilipo, wakague na waonyeshwe risiti za jinsi mzigo ulivyoingia, kama wewe umeingiza mzigo kihalali, kwa nini uone kero Afisa wa serikali kuja kuikagua?

Serikali isirudi nyuma katika hilo. Tunaona wamachinga Wana mzigo wanauza, kumbe wanatoa katika stoo ya tajiri, na tajiri anakuwa kauingiza kimagendo.

Kila mtanzania alipe Kodi, tunataka maendeleo, yatakuja vipi bila Kodi?

Nawashauri TRA hiyo kariakoo waiweke katika maeneo madogo madogo ya kiutawala. Iwe special zone. Wanauza bila risiti, waachwe tu? Hapana.

Huyo kiongozi wao serikali im-pin down kwa uhujumu uchumi, na biashara zake zikione Cha moto
 
Kama wewe sio mfanyabiashara achana na mambo yasiokuhusu.

sijui umeandika nini maana sijasoma ila ungejua jinsi kodi kubwa na double taxation inavyotudidimiza wafanyabiashara apa bongo ungefuta huu uzi.

btw, izo kodi unazotaka watu walipe zinasaidia nini taifa zaidi ya kunufaisha mafisadi to the extent ambayo nchi inaendeshwa kwa Mikopo na sio kodi?
 
E1AECCF2-3A0E-44A7-8A03-215D3CCA0157.jpeg




Ukisikiliza malalamiko mengine ya wafanyabiashara utadhani wanaonewa kweli, wakati utaratibu upo kwenye sheria.

TRA awana mamlaka yeyote nje ya hiyo sheria na mipaka yao ya kazi inaishia hapo; utegemei mfanyabiashara ajue hayo mambo (but it’s good idea to understand) ila kwa ushauri tu wa muhasibu aliesomea kodi ni rahisi kumuelezea jinsi ya kujilinda.

The only logical explanation ya mfanyabiashara kulalamika TRA kutaka access ya storage kuangalia inventory; ni kwamba yeye mwenyewe ajifanyii ata internal audit.

Mamlaka ya kodi ikitaka kuona uwadhulumu kodi yao watataka hiyo access ndio maana kwenye sheria hiyo hiyo kuna section inataka utunze sales receipts and purchases invoices.

Shida kubwa ni uelewa wa maswala ya uhasibu, na haya ni mambo basic tu ya bookkeeping unaweza jifunza ata kwa miezi sita tu.

Yaani huu upuuzi kabisa wa kusimamisha shughuli za bunge kwa uzembe wa wafanyabiashara kutoelewa sheria ya majukumu na kazi za TRA.

Ila hilo la kukamata wateja kwakweli ni ushamba.

Banana republic na wafanyabiashara wenye uelewa mdogo.

Hiyo sheria ya tax administration act; nadhani karibu nchi zote duniani utakuta zina elements hizo hizo. Ni muhimu kwenye sio kwenye kukagua kodi tu ata kwenye materiality in auditing,
 
Huko kwenye maghala kuna bidhaa nyingi ambazo zinapitishwa bila kulipiwa kodi, tra wanaziadiana ndio maana wameamua kwenda kwenye hayo maghala ili kupanua wigo wa ulaji.
Mambo yatakuwa yaleyale, unakutwa na mzigo wa m50, unaambiwa lipa m10 wanasema umekutwa na mzigo wa m15 mambo yanaisha.
 
Huko kwenye maghala kuna bidhaa nyingi ambazo zinapitishwa bila kulipiwa kodi, tra wanaziadiana ndio maana wameamua kwenda kwenye hayo maghala ili kupanua wigo wa ulaji.
Mambo yatakuwa yaleyale, unakutwa na mzigo wa m50, unaambiwa lipa m10 wanasema umekutwa na mzigo wa m15 mambo yanaisha.
Hahahaha Tz ngumu aiseee, manake wafanyabiashara nao wanaona wakwepe kutoka risiti,Ili warudishe kile wanachoumizwa kutokana na rushwa za mzigo bandarini.... upande mwingine wabunge asilimia kubwa ya pesa yao 12 million haikatwi Kodi, na upande mwingine kula CAG analalamika ubadhilifu wa mabilioni serikalini....naona Sasa kila mtu ale kwa kamba yake.....kaazi kwelikweli, na naona tutafika tumechooka sana......
 
Wafanyabiashara walipe kodi waache kutaka mteremko!

Nchi hii wafanyabiashara hawalipi kodi stahiki

Hata EFD wanacheza nazo!

Serikali isimame kidete!
Kabla hujaishauri serikali yako isimame kidete na wafanya biashara ungeishauri isimame kidete na wezi wa Kodi za wananchi ndipo hata mfanya biashara atalipa Kodi bila shuruti
 
Hivi!!? Mathalani nina duka ambalo halitoshelezi mzigo hivyo nikachukua store kwaajili ya kuhifadhi mizigo yangu, nayo nailipia kodi!!!? Kama nini!!? Inakua na leseni ya biashara kama duka!!? Wizi hautoisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom