Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Kwenye tax administration act section 35 and 36 is not out of blue that’s just everyday booking. Bila ya ata uwepo wa hiyo sheria kibiashata tu it’s good practice ili usipigwe na wafanyakazi wako unahitaji kutunza hizo evidence anyway.Upo sawa mkuu mfumo bora unahitajika, mfanyabiashara haiangalii biashara kwa jicho la kiasibu, anaiangalia kwa jicho la kibiashara na hana matumizi na hesabu sababu yeye anatazama faida kwa jicho tofauti na accounting profit ila analazimika kuwa na hesabu sababu ya TRA na Banks.
Wakati mhasibu akiwaza cost of sales, Asset & Liabilities, cashflow and ratios mfanyabiashara yeye anachukua alichoingiza toa alichogharamia kupima iwapo biashara inalipa au la.
Wakati mhasibu akiwaza ROI, SWOT, Projected cashflow and feasibility reports, Mfanyabiashara anafikiria kupeleka pesa bank, kuongeza mzunguko, awe na collateral kisha akopesheke aongeze mzigo maana ameshaona unahitajika na kina nani.
Watu wawili, field moja ila fikra tofauti kabisa. Mara nyingi mfanyabiashara anamuona mhasibu kama mtu anayekula pesa zake bure. Kama sio bank na TRA kuhitaji mahesabu huenda asingemtaka kabisa.
Ukija kwenye Kodi. Kodi ni sheria sio uhasibu mfanyabiashara anahitaji kujua tu sheria inamtaka afanyaje ili aendelee kufanya biashara na hapa ndipo umuhimu wa mfumo bora unapozidi kuonekana. Mfumo ambao utakata kodi halali na TRA na mfanya biashara wasiviziane.
In bookkeeping:
Unahitaji ku record sales receipts ku record mauzo. Unahitaji purchase receipt kudai vat.
Hizo evidence zinakusaidia ku trace inventory, kufanya bank reconciliation kuangalia hela iliyopo bank ipo sawa kutokana na manunuzi yako na mauzo yako ya biashara na faida iliyopo au hasara.
Part V ya administration act inaweka tu msisitizo wa kutunza hizo accounting receipts kwa sababu na wao TRA wanatumia vielelezo hivyo hivyo kwenye kukudai kodi au unapowadai wewe kodi (kwa sababu kama unalipa in accrual kwa makadirio yao, mwisho wa mwaka si ajabu wewe ukawa unawadai inabidi wakurudishie and interest juu kadri wanavyochelewa kukupa.
Kama nilivyosema awali hakuna jipya kwenye hiyo sheria because ina elements za booking tu, sema hizo info pia ndio zinazotumika kwenye tax investigation.
Sasa ukiona mfanyabiashara analalamikia process za TRA sio kwamba hajui sheria tu il ni kwamba ata uelewa wake wa maswala ya bookkeeping ni tatizo.
Pili nimemsikiliza waziri mkuu kuhusu hoja za storage, story ni ndefu na malalamiko ya wafanyabiashara yana elements zilezile uelewa mdogo kuhusu storage and how inventory could be traced. Lakini tatizo sio wafanyabiashara wa Kariakoo bali hao watu wanaowaagizia mizigo kuna mashehena inaonekana yanapita bandarini bila ya kulipiwa kodi, ukijumlisha mzigo wenyewe ni bulk ya wafanyabiashara tofauti hiko ni kimeo kwao TRA wakitaka kuona mzigo wao kwa sababu awawezi kuwa na hizo receipts za clearance bandarini.
Ni swala dogo sana kulitatua iwapo hao wafanyabiashara wanapewa receipt za manunuzi kwa huyo shipper wao it can be traced; hawana kwa sababu kuna ukwepaji wa kodi kwenye kuingiza mizigo bandarini. Nyuma ya huo mgomo wa leo kuna mafisadi bandarini na Zungu ni sehemu ya hiyo team ya mafisadi.
TRA are not stupid wakiamua