Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

bossi ukiambiwa ukatoe ushahidi utaweza?!, we unafanya biashara gani mkuu?!, kama unasubiri notification ya bank mwisho wa wezi huwezi elewa kero na karaha. wanazopitia. itoshe kusema kuwa mazingira ya kodi yanatakiwa kuwa rafiki kwa mlipaji.
Kwani mizigo inaingia na meli au Manuari!? Kama ni meli si bandari ndio mzigo inapokelewa!? Sasa huu uzushi unautoa wapi!?
 
Nadhani malalamiko yao umeyasikiliza vizuri..
Issue siyo kulipa Kodi ni taratibu wanazotimia kukusanya/kupata hizo kodi...

Kulipa si wanalipa miaka yote...Tena kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo siyo Issue..
Kwani wao ulipaji wa kodi ni tofauti na wafanyabiashara wengine?inshu sio utaratibu hawataki kutumia EFD,kwani wengi hawapendi kuandika thamani halisi ya mauzo,na ndio maana kariakoo kuna watumishi wa TRA wao ni kufuatilia wateja,wanaokuwa wamenunua bidhaa,na unakuta mtu ana tv ya thamani ya laki 6,ila risiti aliyonayo imeandikwa laki 2!
Na usajiri wa store ndio umewavuluga mnooo!!
 
Ukweli ni kwamba kuna tatizo, fuatilia rapid open interview aliyoifanya Mkuu mpya mteule wa Mkoa alipokuwa akiongea na sampuli ya wafanyabiashara.
 
Hospital za nje ukienda kutibiwa wanakutibu lakini wanenda mbali kuangalia nini imeleta hali hiyo ili watibu kule pia sasa badala ya ku deal na matokeo kwanini wasiende na kuangalia inapitaje kwenye mfumo wote huo bila kulipa kodi, je wana bypass system, je kuna bandari bubu, je kuna airport bubu, je mipaka haiko salama kuna maswali mengi sana na kwanini wafanya biashara wanafanya wanayofanya je wanahisi wanaonewa kodi kubwa hazilipiki ni lazima jambo hili liangaliwe katika package ya kukuza uchumi kwa miaka mingi haya mambo hayawezi kuamuliwa kwenye kikao kimoja tu leo, ni lazima tuje na package ya kuchochea ukuaji wa uchumi na kufanya Tz kuwa kitovu cha biashara EA na haya yanawezekana.
 
Wabongo hasa wachaga wanapenda mtelezo

USSR

Sent using Jamii Forums mobile
Dah! Unaonesha ulivyojaa chuki dhidi ya kabila ulilolionesha hapo juu.
Najiuliza hivi ni kweli hususani ulipoandika hasa wachaga?. Kwa nini umewachukulia kama case study?.Tafsiri yangu juu ya mstari uliouandika ni kwamba wabongo wengi wanapenda njia rahisi lakini Wachaga wao wanapenda zaidi. This is more than a fallacy of hasty generalizations.
..................................................................................................
 
Mfanyabiashara anayo haki ya kuclaim Input tax aliyolipia wakati akifanya importation kama amefanya taxable supplies na amesajiliwa VAT. Sheria inatoa haki kwa pande zote mbili.. ila Wafanyabiashara wengi ni wabinafsi wanataka mapato yote yabaki kwao.. Sheria haimkandamizi mfanyabiashara.. inampa uhuru wa kuandaa vitabu vyake mwenyewe na kujikadiria kodi mwenyewe... kufile for VAT mwenyewe ila They are not faithfully.
Kwanin hawako faithful unadhan the only reason ni roho ya kutaka kingi ?

Sio mfanyabiashara niliesimama ila nipo kweny huo ulimwengu nahakika 90% wapo tayar kulipa kodi shida ni hio serikali.

Kaka unaongelea inshu ya kuclaim,em niambie kuhusu input na output taxes na jinsi ya kuclaim labda sijui.
 
Tuna Utaratibu mbovu sana wa ulipaji Kodi nchini infact ukifuatiia hata ukadiriaji wa kodi unaofanywa na watu wa TRA kwenye maduka matatu tu yaliyopo hata mtaani unapoishi utabaini magumashi.
Makadirio magumashi, ulipaji magumashi..
 
Upo sawa mkuu mfumo bora unahitajika, mfanyabiashara haiangalii biashara kwa jicho la kiasibu, anaiangalia kwa jicho la kibiashara na hana matumizi na hesabu sababu yeye anatazama faida kwa jicho tofauti na accounting profit ila analazimika kuwa na hesabu sababu ya TRA na Banks.

Wakati mhasibu akiwaza cost of sales, Asset & Liabilities, cashflow and ratios mfanyabiashara yeye anachukua alichoingiza toa alichogharamia kupima iwapo biashara inalipa au la.

Wakati mhasibu akiwaza ROI, SWOT, Projected cashflow and feasibility reports, Mfanyabiashara anafikiria kupeleka pesa bank, kuongeza mzunguko, awe na collateral kisha akopesheke aongeze mzigo maana ameshaona unahitajika na kina nani.

Watu wawili, field moja ila fikra tofauti kabisa. Mara nyingi mfanyabiashara anamuona mhasibu kama mtu anayekula pesa zake bure. Kama sio bank na TRA kuhitaji mahesabu huenda asingemtaka kabisa.

Ukija kwenye Kodi. Kodi ni sheria sio uhasibu mfanyabiashara anahitaji kujua tu sheria inamtaka afanyaje ili aendelee kufanya biashara na hapa ndipo umuhimu wa mfumo bora unapozidi kuonekana. Mfumo ambao utakata kodi halali na TRA na mfanya biashara wasiviziane.
Jamaa una akili wewe. Ningekua kwenye mamlaka za uteuzi ungeongoza kitengo. Kuna vijamaa vimekariri madesa vinaona wafanyabiashara hawana akiliiii
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
.Jamaa una akili wewe. Ningekua kwenye mamlaka za uteuzi ungeongoza kitengo. Kuna vijamaa vimekariri madesa vinaona wafanyabiashara hawana akiliiii
😀 😀 shukran sana mkuu kwa hilo.
 
Wafanyabiashara wengi wanaunga unga mitaji hawawezi kuleta kontena zima.

Wanajiunga kikundi wanamtuma mmoja mzigo unaingia kwa jina moja.

Wakishapeana kila mtu wa kwake wanajikuta hawana risiti mzigo unageuka wa magendo wazalendo uchwara wanawaita wakwepa kodi.
Hii ni sababu ya msingi
 
Mmekalia ofisi ma mishahara makubwa siku za kustaaf zikifika mtaani mnapashindwa.Mnabakia kufuga kuku.Acheni viburi tengenezeni mazingira mazuri ya Biashara hata nyinyi yatakuja kuwasadia
 
Nataman nikutukane pumbavu zako. Wew unadhan watu hawapendi kulipa kodi?

Unadhan watu wanapenda kuingiza mizigo kimagendo?
Kwani kuingiza mizigo ya magendo inalazimishwa? Watu wanataka utajiri wa harakaharaka. Siamimi kama wafanyabiashara pamoja na malalamiko yao yooote wao hawana sehemu ya kulaumiwa.
 
Nilitamani sana TRA, TPA, POLISI nao wapewe platform wajibu tuhuma zao publically ili ku balance story. Siamini kama Wafanyabiashara ni wasafi kivile, ila mtu ana upande wake wa pili wa shillingi
 
wana vitu vingi vya magendo hupitisha baharini na kuna vitu kama vipodozi vilivyopigwa marufuku wao wanazo stoo
 
Yaani nipewe makadirio ya stoo na y dukani?
 
Kwani kuingiza mizigo ya magendo inalazimishwa? Watu wanataka utajiri wa harakaharaka. Siamimi kama wafanyabiashara pamoja na malalamiko yao yooote wao hawana sehemu ya kulaumiwa.
Kaka hizi biashara kama kamishna wa TRA na wasaidizi wake wakiazimia kila bidhaa ilipe kodi watu watalipa bila shida. Mim naingiza bidhaa × ila kodi nayolipa hailingani na mtu mwingine alieingiza alike products ,unafikir margin yetu itakua sawa. Unafikir next time nkitak kuingiza mzigo nini ntafanya?

Mfano naingiza IST kodi nayotakiwa kulipa ni 3M fine nalipa yote.Mwingne anaingiza IST lakini kodi analipa kimagumashi unafikir huko sokoni nan atauza hio IST haraka
 
Wafanyabiashara wengi wanaingiza mizigo kwa njia ya magendo, wanazitunza stoo. Wanaweza kupitishia bandarini, njia zisizo rasmi za mipakani, au kwa majahazi. Hawalipi Kodi.

Sasa serikali imeamua kusajili stoo wanazotunzia ili waweze kujua zilipo, wakague na waonyeshwe risiti za jinsi mzigo ulivyoingia, kama wewe umeingiza mzigo kihalali, kwa nini uone kero Afisa wa serikali kuja kuikagua?

Serikali isirudi nyuma katika hilo. Tunaona wamachinga Wana mzigo wanauza, kumbe wanatoa katika stoo ya tajiri, na tajiri anakuwa kauingiza kimagendo.

Kila mtanzania alipe Kodi, tunataka maendeleo, yatakuja vipi bila Kodi?

Nawashauri TRA hiyo kariakoo waiweke katika maeneo madogo madogo ya kiutawala. Iwe special zone. Wanauza bila risiti, waachwe tu? Hapana.

Huyo kiongozi wao serikali im-pin down kwa uhujumu uchumi, na biashara zake
Sawa Nchemba. Tatizo hata kodi zikilipwa Mnaishia kuzipiga.. Makodi makubwa af yanaishia kusikojulikana.
 
Wanapitisha mizigo kwa majahazi kutoka Zanzibar wanashushia Bagamoyo na Tanga, Niliwahi kushuhudia Lori limebeba vifaa vya kielekroniki, usiku, wanapita chocho kwa chocho. Wamevitoa Kenya.

Border ya Ngara, mugoma huko, fuso zinashusha bia za Burundi usiku mnene, bodaboda zinapokea na kuingiza mitaani kwenye stoo za wafanya biashara, bado vitenge Kila siku vinakamatwa.

Samia mnamlilia maendeleo, mara miradi inachelewa, kumbe mtu ana stoo ya mabilioni halafu mzigo wote wa magendo.
Hivi haya yote yanafanyika ulinzi na usalama unakuwa umelala.Na kwanini ukuwai kituo cha usalama cha karibu waende kukamata hayo magendo.
 
Back
Top Bottom