Point muhimu hapo ni hiyo ya TRA kuwafahamu wafanyabiashara wao na kutoa elimu zaidi.
Another alternative inayoleta shida ni kukosekana kwa accounting services Tanzania. Nchi nyingi duniani biashara ambazo hazina uwezo wa kuajili accountant full time. Unaweza pata huduma za kihasibu periodically kwa sababu ya hesabu kodi na ushauri wa maswala ya kodi.
Vinginevyo umenunua mzigo 10 elewa kodi ya kwanza hapo ni VAT hiyo ipo unapouza tu, pili kuna kodi ya faida (income tax) hiyo sasa kabla ujalipa ndio unatoa gharama za kusafirisha migo unaweza kuwa ata umetengeneza hasara usidaiwe. Kwenye hasara unaruhusiwa kupata tax rebate (kurudishiwa baadhi ya hela ulizolipia income tax miaka ya nyuma na TRA).
Ni hivi swala la kodi ni uelewa wa taratibu za kiuhasibu na upo kundi gani; vinginevyo viwango vya kodi ni sheria ambayo baadhi vinaweza badilika kila mwaka kutokana na budget.
Na administration ya kodi (jinsi hiyo kodi) itakavyodaiwa TRA pia wanasheria yao ya mwongozo; awawezi fanya kinyume na hapo.
Wajibu wa mlipa kodi kwenye sheria ni kuelewa hasa
View attachment 2623103
View attachment 2623105
Muhimu kwa mfanyabiashara ni kuelewa ‘section V’ yote ya tax administration nimeweka baadhi ya mambo humo yanayoelezea nini cha kutunza kwenye vitabu na power of access waliyo nayo TRA.
Shida zaidi ni maafisa hao maafisa wa TRA na wengine ni vigogo ata wao hiyo sheria sijui awajailewa. Kuna wasaa unawasikia wanawaambia watu sio lazima kutunza vitabu kwa sababu mauzo yao ayajafika 100 million. Hakuna sehemu sheria inasema hivyo. Ata kama viwango vya kodi ni tofauti na malipo yako ni tofauti, swala la kutunza hesabu sahihi ni la kisheria na kwa usalama wako.