Serikali huduma zake nyingi haigharamii, kwahiyo wahusika wanatumika pesa zao kuendesha hizo huduma. Na Mbadala wake ndio wananiongeza hivyo.
Mfano:
- Mtendaji wa kijiji, hapewi stationery, usafiri au Mafuta na hapo unategemea huduma za mihuri na barua ziwe bure
- Vituo vya polisi wanatakiwa kulisha mahabusu, kuwasafirisha kwenda Mahakamani na Kama Askari hawatoshi ukodi mgambo, na budget hawana.
- Ofisi nyingi za serikali hazina Bando, na Sasa hivi kila siku shughuli za serikali zinataka mtandao. Utajikuta unatumia pesa zako kuweka bando ili utoe huduma za serikali za bure.
Huko Hospitali, utaambiwa kujifungua ni bire lakini waulize serikali vifaa vya kunifungukia (delivery kits) huwa wanapeleka.
Mwisho serikali haijawahi kuwa na huruma na mtu, utatumika ukifika miaka 60 umeisha, unatelekezwa hapo na Kikokotoo Cha 33% ukafie mbele.
Nchi hii matatizo utosini mpaka kwenye nywewe lakini Wanasiasa wao wana maisha ya mfumo na Daraja tofauti.