Kwanini wafanyakazi wengi wa Serikali wanapenda kutengeneza mazingira ya kupewa hela katika huduma wanazotoa?

Hapo na wewe hukuwa mustaarabu kama umeshakubaliana jambo na mtu ulipaswa ulitende. Usijisifie kwa hilo
 
Wewe unataka tule wapi, hii nchi ilishakwenda na Maji.

Ni wapi hakuna rushwa, Askari barabarani anapokea live bila Chenga unataka sisi tufanye nini
Tatizo lenu wengine mnajipangia hadi bei kubwa kwenye rushwa, mnatakiwa kupokea chochote kile utakachopewa baada ya kazi kama shukrani tu, na kama mteja hana kitu msifanyie ubaya!!
 
Mi nilikuja kupatwa butwaa mwaka huu mwanzoni ..kuna MTU ana kesi Mahakama kuu ..lakini haiendi ..

Kila mwezi tarehe ... Sasa tukiwa kwenye sherehe flani akasikia MTU anasema nilimaliza kesi yangu miezi 6 tuu .. Ikabidi aombe maelezo kwa mhusika ..
Akaambiwa ni pesa yako ndio inamaliza kesi mapema ..

Huwezi amini pesa kwa hapa Bongo inalainisha mambo mengi hasa ofisi za Serikali kwa uharaka ..

Kuna MTU alidai pension kidogo awe kichaa ...ila alipokubali kutoa cha juu ..mwezi haukuisha hela ikaingia kwenye account.. Yaani ni mfumo ndani ya Serikali
 
Ni kutokana na mfumo wa Serikali kuu kuomba omba pesa za misaada.Watoto wakimuona baba na Mama wanapenda kuomba omba na wao hufanya hivo.KAWAIDA NI KAMA SHERIA.
 
Hao TAKUKURU hawafanyi kazi waliopewa kuwasaka waomba rushwa. Wanangoja wapewe ripoti kuwa mahali fulani kuna mazingira ya rushwa ikisha na wao wanajiunga na kuwaomba hao wapokea rushwa wawape gawio lao.
Rushwa imekua ni kitu kinachochukuliwa kama ni sawa katika jamii.
 
ACHA WATU WALE RUSHWA TU

HUKO JUU KWENYEWE WANAPIGA

HELA NDEFU, UNAFIKIRI WACHINI NAYE ATAJISIKIAJE

ova
 
ACHA WATU WALE RUSHWA TU

HUKO JUU KWENYEWE WANAPIGA

HELA NDEFU, UNAFIKIRI WACHINI NAYE ATAJISIKIAJE

ova
Sasa hawa watumishi wa chini wao wanawaumiza sana wanyonge, sasa mtu kazulumiwa shamba lake na tajiri anaambiwa atowe pesa ili apewe msaada sasa huyo mnyonge hiyo pesa atapata wapi!?
 
Kma viongoz wanapatikana kwa mchakato wa rushwa
Your browser is not able to display this video.
 
Yaani wee acha tu maana imebidi sasa nimwombe Mungu maana haki yako upati mpka utoe rushwa. Nimefuatilia hati ya kiwanja changu kwa zaidi ya miaka ishirini bila mafanikio. Huko pembeni unaambiwa bila kuto chochote upati na ni kweli kila ukienda wanakuwekea mazingira ya rushwa. . Baadaye nikaamua tu kuwaachia mpaka hapo watakapoona wenyewe kunipa au Mungu afanye ukuu wake apindue mambo na kuleta watu wanaojali watu. Kwa sasa hivi maskini anapata shida sana nchi hii maana kupata haki ni majaliwa. Mungu anawaona ninyi nyote mnaofanya dhuluma mwogopeni Mungu angalau basi. Pesa mnazokusanya hamwezi kwenda nazo kaburini na hayo majumba manayojengwa kwa rushwa hamtakaa na watoto wenu watatafunwa na laana. Ole wenu ninyi nyote mnaopindisha haki za watu maana Mungu hatakapoamua kuwaweka uchi mtakuwa uchi kwekweli.
 
Kuna vitu vingine huwa nasi tunavitaka wenyewe. Sasa hapo TRA wameshaweka TIN bure mtu anakuambia nipe kitu kidogo kwanini usimuione mkuu wake hapo au hata CG wao Kidata uone huyo muomba rushwa nini kitamkuta. Bora TRA wao wamewapa somo TIN bure bango lipo na inashangaza na wewe unakubali , tatizo naliliona na sisi tunachangia kutaka vitu kwa haraka hasa unapokuta wenzako wamekutangulia kwenye foleni. Mimi Ardhi kuna mtu alitaka mazingira ya kunitoa Rushwa nikamtafuta naibu waziri mbona jamaa jasho lilimtoka kila akiniona nyaraka yangu faster mara ooooh ilikuwa haina haja ya kwenda huko tungeyamaliza nilimjibu nishamaliza. Dawa ni kuwaripoti tuu na niwapongeze TRA kwa kuweka matangazo hayo
 
alafu wanataka waende mbinguni na madhambi yote wayafanyayo...wazinzi wenyewe, wezi wenyewe, waongo wenyewe, wapenda rushwa wenyewe, n.k hovyo kabisa
 
umemaanisha mimi nilikubali kutoa kitu kidogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…